Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za ajira mpya kufuatia kibali cha ajira Kumb. Na. FA/97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili 2025 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1.0 DEREVA DARAJA LA II β NAFASI 15
1.1 Majukumu ya Kazi
-
Kukagua gari kabla na baada ya safari.
-
Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi.
-
Kufanya matengenezo madogo ya gari.
-
Kukusanya na kusambaza nyaraka.
-
Kutunza taarifa za safari kwenye daftari la safari.
-
Kufanya usafi wa gari.
-
Kufanya kazi nyingine kwa maelekezo ya msimamizi.
1.2 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
-
Leseni ya Daraja E au C; awe ameendesha kwa mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
-
Cheti cha mafunzo ya msingi ya Udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS B1.
2.0 Masharti ya Jumla kwa Waombaji
-
Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
-
Kuambatisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na mwanasheria au wakili.
-
Kuambatisha Curriculum Vitae yenye mawasiliano na wadhamini 3.
-
Kuambatisha vyeti vya taaluma na elimu vilivyothibitishwa.
-
Testimonial, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips hazitakubaliwa.
-
Vyeti vya waliosoma nje vihakikiwe na TCU, NECTA au NACTE.
-
Waliofukuzwa au kustaafishwa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali.
-
Waajiriwa wa Umma walioko kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.
-
Wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na waeleze aina ya ulemavu kwenye mfumo.
-
Wenye tofauti ya majina waambatanishe DEED POLL.
-
Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
-
Waombaji walioteuliwa kwa usaili wanashauriwa kuvaa mavazi yanayozuia baridi kutokana na hali ya hewa ya Arusha.
-
Mwisho wa kutuma maombi: 25 Juni 2025.
-
Barua ya maombi iandikwe kwa:
Mkurugenzi,
Halmashauri ya Jiji la Arusha,
S.L.P 3013, 20 Barabara ya Boma, 23101 ARUSHA.
-
Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia: https://portal.ajira.go.tz
Imetolewa na:
Dr. Nindwa Maduhu
KAIMU MKURUGENZI WA JIJI β HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA
Makala Nyingine:
Tuachie Maoni Yako