Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kujaza nafasi za ajira mpya kufuatia kibali cha ajira Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili 2025 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II β NAFASI 2
1.1 Majukumu ya Kazi
-
Kuorodhesha barua zinazoingia na zinazotoka.
-
Kusambaza na kurudisha majalada kwa watendaji.
-
Kutafuta na kurudisha nyaraka sehemu husika.
-
Kufuatilia mzunguko wa majalada (File Tracking).
1.2 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).
-
Stashahada (Diploma β NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
-
Awe na ujuzi wa kompyuta.
1.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS C.
2.0 DEREVA DARAJA LA II β NAFASI 4
2.1 Majukumu ya Kazi
-
Kukagua gari kabla na baada ya safari.
-
Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi.
-
Kufanya matengenezo madogo ya gari.
-
Kukusanya na kusambaza nyaraka.
-
Kutunza taarifa za safari kwenye daftari la safari.
-
Kufanya usafi wa gari.
2.2 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
-
Leseni ya Daraja E au C; ameendesha kwa mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
-
Cheti cha mafunzo ya msingi ya Udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
2.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS B.
3.0 MUHUDUMU WA JIKONI DARAJA LA I β NAFASI 2
3.1 Majukumu ya Kazi
-
Kusafisha vyombo vya kupikia na vya kulia chakula.
-
Kusafisha meza za chakula na maeneo ya kulia na kupikia.
-
Kuwatayarishia wapishi vifaa vya kupikia na mezani.
-
Kuwasaidia waandazi na wapishi katika maandalizi ya chakula.
3.2 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
-
Uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu.
3.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGOS A.
4.0 MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMII DARAJA LA II β NAFASI 4
4.1 Majukumu ya Kazi
-
Kusaidia kubuni na kupanga mipango na miradi ya maendeleo.
-
Kushiriki katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
-
Kutoa elimu ya kujitegemea kwa jamii.
-
Kutoa taarifa za kazi za maendeleo kwa uongozi wa kijiji na msimamizi wake.
-
Kusaidia kuunda vikundi vya jamii na kusaidia kaya masikini kutumia fursa za maendeleo.
4.2 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
-
Astashahada (Certificate) ya Maendeleo ya Jamii kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika fani za: Community Development, Sociology, Project Planning and Management, Rural Development au fani zinazofanana.
4.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS B.
5.0 Masharti ya Jumla kwa Waombaji
-
Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
-
Kuambatisha cheti cha kuzaliwa.
-
Kuambatisha Curriculum Vitae yenye mawasiliano na wadhamini 3.
-
Kuambatisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa.
-
Testimonial, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips hazitakubaliwa.
-
Wenye tofauti ya majina waambatishe DEED POLL.
-
Waombaji wa kada ya Dereva waambatishe vyeti vya mafunzo ya Udereva.
-
Kuambatisha picha mbili (passport size) za hivi karibuni.
-
Vyeti vya waliosoma nje vihakikiwe na TCU, NECTA au NACTE.
-
Waliofukuzwa au kustaafishwa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali.
-
Waajiriwa wa Umma walioko kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.
-
Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
-
Mwisho wa kutuma maombi: 01 Julai 2025.
-
Barua ya maombi iandikwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,
S.L.P 42, SINGIDA.
-
Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia: https://portal.ajira.go.tz
Imetolewa na:
Kastori Msigala
MKURUGENZI MTENDAJI β HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI
TANGAZO LA AJIRA IKUNGI DC.pdf
Makala Nyingine:
Tuachie Maoni Yako