Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa stahiki kujaza nafasi za ajira mpya kufuatia kibali cha ajira Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili 2025 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II β NAFASI 4
1.1 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).
-
Stashahada (Diploma) au NTA Level 6 katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
-
Awe na ujuzi wa kompyuta.
1.2 Majukumu ya Kazi
-
Kuorodhesha barua zinazoingia na zinazotoka.
-
Kusambaza na kurudisha majalada kwa watendaji.
-
Kutafuta na kurudisha nyaraka katika sehemu husika.
-
Kufuatilia mzunguko wa majalada (File Tracking).
1.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS C1.
2.0 DEREVA DARAJA LA II β NAFASI 4
2.1 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
-
Leseni ya Daraja E au C, awe ameendesha kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
-
Cheti cha mafunzo ya msingi ya Udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
2.2 Majukumu ya Kazi
-
Kukagua gari kabla na baada ya safari.
-
Kuwapeleka watumishi katika safari za kikazi.
-
Kufanya matengenezo madogo ya gari.
-
Kukusanya na kusambaza nyaraka.
-
Kutunza taarifa za safari katika daftari la safari.
-
Kufanya usafi wa gari.
2.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS B1.
3.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II β NAFASI 5
3.1 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
-
Stashahada (Diploma) au NTA Level 6 ya Uhazili.
-
Kuwa amefaulu somo la Hatimkato (Shorthand) ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja.
-
Awe na ujuzi wa Programu za Ofisi za Kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail, Publisher).
3.2 Majukumu ya Kazi
-
Kuchapa barua, taarifa na nyaraka mbalimbali.
-
Kupokea wageni na kuwahudumia.
-
Kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, safari, na ratiba za vikao.
-
Kutafuta na kusambaza majalada kwa maofisa husika.
-
Kupanga dondoo na kuandaa vikao mbalimbali.
-
Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
3.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS C1.
4.0 Masharti ya Jumla kwa Waombaji
-
Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
-
Wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na kueleza aina ya ulemavu kwenye mfumo.
-
Kuambatisha Curriculum Vitae yenye maelezo ya mawasiliano na wadhamini 3.
-
Kuambatisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na mwanasheria au wakili.
-
Testimonial, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips hazitakubaliwa.
-
Vyeti vya waliosoma nje vihakikiwe na TCU, NECTA au NACTE.
-
Waliofukuzwa au kustaafishwa katika utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali.
-
Waajiriwa wa Umma walioko kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.
-
Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
-
Waombaji wa nafasi za Dereva II waambatishe vyeti vya mafunzo ya Udereva.
-
Majina yanayofautiana yaambatane na DEED POLL.
-
Mwisho wa kutuma maombi: 29 Juni 2025.
-
Barua ya maombi iandikwe kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA NGORONGORO
S.L.P 1, LOLIONDO
-
Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia: https://portal.ajira.go.tz
Imetolewa na:
Murtallah S. Mbillu
MKURUGENZI MTENDAJI, HALMASHAURI YA WILAYA YA NGORONGORO
.pdf TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NGORONGORO 16-06-2025
Makala Nyingine:
Tuachie Maoni Yako