Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za ajira mpya baada ya kupokea kibali Kumb. Na. FA.97/288/01/25 cha tarehe 29 Aprili 2025 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II β NAFASI 4
1.1 Majukumu ya Kazi
-
Kuorodhesha barua zinazoingia na zinazotoka.
-
Kusambaza na kurudisha majalada kwa watendaji.
-
Kutafuta na kurudisha nyaraka sehemu husika.
-
Kufuatilia mzunguko wa majalada (File Tracking).
-
Kufanya kazi nyingine kwa maelekezo ya msimamizi wake.
1.2 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).
-
Stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
-
Awe na ujuzi wa kompyuta.
1.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS C.
2.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II β NAFASI 4
2.1 Majukumu ya Kazi
-
Kuchapa barua, taarifa na nyaraka mbalimbali.
-
Kupokea wageni na kuwaelekeza sehemu sahihi.
-
Kutunza kumbukumbu za matukio, vikao, safari na miadi.
-
Kutafuta na kusambaza nyaraka kwa maofisa husika.
-
Kupanga dondoo na maandalizi ya vikao mbalimbali.
-
Kuandaa orodha ya vifaa vya ofisi.
2.2 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).
-
Stashahada (Diploma) au NTA Level 6 ya Uhazili.
-
Kuwa amefaulu Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja.
-
Ujuzi wa programu za kompyuta za ofisi (Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail, Publisher).
2.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS C.
3.0 DEREVA DARAJA LA II β NAFASI 5
3.1 Majukumu ya Kazi
-
Kukagua gari kabla na baada ya safari.
-
Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi.
-
Kufanya matengenezo madogo ya gari.
-
Kutunza na kuandika taarifa za safari (log book).
-
Kukusanya na kusambaza nyaraka.
-
Kufanya usafi wa gari.
-
Kufanya kazi nyingine kadri ya maelekezo ya msimamizi.
3.2 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
-
Leseni ya Daraja E au C; awe ameendesha kwa mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
-
Cheti cha mafunzo ya msingi ya Udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
3.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS B.
4.0 Masharti ya Jumla kwa Waombaji
-
Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
-
Wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na waeleze aina ya ulemavu kwenye mfumo.
-
Kuambatisha Curriculum Vitae yenye maelezo ya mawasiliano na wadhamini 3.
-
Kuambatisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na mwanasheria au wakili.
-
Testimonial, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips hazitakubaliwa.
-
Waajiriwa wa umma walio na sifa mpya wapitishe maombi yao kwa waajiri wao.
-
Vyeti vya waliosoma nje vihakikiwe na TCU, NECTA au NACTE.
-
Waliofukuzwa au kustaafishwa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali.
-
Waajiriwa wa Umma walioko kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.
-
Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
-
Dereva II waambatishe vyeti vya mafunzo ya Udereva.
-
Tofauti ya majina lazima iambatishwe na DEED POLL.
-
Mwisho wa kutuma maombi: 29 Juni 2025.
-
Barua ya maombi iandikwe kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
S.L.P 70, SIKONGE.
-
Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia: https://portal.ajira.go.tz
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI (W) β SIKONGE
Makala Nyingine:
Tuachie Maoni Yako