Majina ya Walimu Walioitwa Kazini 2025/2026 Kupitia Ajira Portal (orodha na list ya majina kwenye PDF walioajiriwa 2025 na vituo vyao vya kazi) Majina ya walimu waliopata kazi 2025 MAJINAYA WALIOITWA KAZINI WALIMU KADA ZA UALIMU.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 14-08-2024 na tarehe 17-01-2025 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili.
Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Majina ya Walimu Walioitwa Kazini 2025
Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite
kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.
MUHIMU:
Wanaokuja kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi wanapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:-
- Kitambulisho cha Uraia,
- Hati ya kusafiria,
- Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi,
- Kitambulisho cha Mpiga kura au
- Leseni ya Udereva.
Orodha Ya Majina Kamili:
Kwa taarifa zaidi tembelea; https://www.ajira.go.tz/
Makala Nyingine:
- Majina Ya Walioitwa Kazini Utumishi Na Ajira Portal 2025
- Majina Ya Waliopata Ajira Kada Ya Afya Oktoba 18, 2024
- Matokeo Ya Usaili Wa Kuandika Mwalimu Daraja La Iii b (kemia, Baiolojia,tehama, Jiografia) Na Mwalimu Daraja La Iiia Elimu Ya Awali
- Matokeo Ya Usaili Wa Kuandika Mwalimu Daraja La III C Kiswahili
- Ratiba Ya Usaili wa Walimu 2025 (Kada Za Ualimu)
- Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI Na Ajira Portal 2025
- Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato cha nne 2024 (form Four)
- Matokeo ya Usaili Ajira Portal 2025, Matokeo ya Utumishi wa Umma, Serikalini
Mimi jamani mbona sijapangwa na nilihitimi chuo 2016??Nisaidieni na Mimi mtoto wa mkulima hata mlo mmija ni shida.
ulisoma masomo yapi?
Mbona ualimu daraja la IIIA, hayaonekani?