Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Ikungi Juni, 2025

Filed in Ajira by on June 21, 2025 0 Comments

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kujaza nafasi za ajira mpya kufuatia kibali cha ajira Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili 2025 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

1.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 2

1.1 Majukumu ya Kazi

  • Kuorodhesha barua zinazoingia na zinazotoka.

  • Kusambaza na kurudisha majalada kwa watendaji.

  • Kutafuta na kurudisha nyaraka sehemu husika.

  • Kufuatilia mzunguko wa majalada (File Tracking).

1.2 Sifa za Mwombaji

  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).

  • Stashahada (Diploma – NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

  • Awe na ujuzi wa kompyuta.

1.3 Mshahara

  • Ngazi ya mshahara TGS C.

2.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 4

2.1 Majukumu ya Kazi

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari.

  • Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi.

  • Kufanya matengenezo madogo ya gari.

  • Kukusanya na kusambaza nyaraka.

  • Kutunza taarifa za safari kwenye daftari la safari.

  • Kufanya usafi wa gari.

2.2 Sifa za Mwombaji

  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).

  • Leseni ya Daraja E au C; ameendesha kwa mwaka mmoja bila kusababisha ajali.

  • Cheti cha mafunzo ya msingi ya Udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.

2.3 Mshahara

  • Ngazi ya mshahara TGS B.

3.0 MUHUDUMU WA JIKONI DARAJA LA I – NAFASI 2

3.1 Majukumu ya Kazi

  • Kusafisha vyombo vya kupikia na vya kulia chakula.

  • Kusafisha meza za chakula na maeneo ya kulia na kupikia.

  • Kuwatayarishia wapishi vifaa vya kupikia na mezani.

  • Kuwasaidia waandazi na wapishi katika maandalizi ya chakula.

3.2 Sifa za Mwombaji

  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).

  • Uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu.

3.3 Mshahara

  • Ngazi ya mshahara TGOS A.

4.0 MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMII DARAJA LA II – NAFASI 4

4.1 Majukumu ya Kazi

  • Kusaidia kubuni na kupanga mipango na miradi ya maendeleo.

  • Kushiriki katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

  • Kutoa elimu ya kujitegemea kwa jamii.

  • Kutoa taarifa za kazi za maendeleo kwa uongozi wa kijiji na msimamizi wake.

  • Kusaidia kuunda vikundi vya jamii na kusaidia kaya masikini kutumia fursa za maendeleo.

4.2 Sifa za Mwombaji

  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).

  • Astashahada (Certificate) ya Maendeleo ya Jamii kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika fani za: Community Development, Sociology, Project Planning and Management, Rural Development au fani zinazofanana.

4.3 Mshahara

  • Ngazi ya mshahara TGS B.

5.0 Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  1. Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.

  2. Kuambatisha cheti cha kuzaliwa.

  3. Kuambatisha Curriculum Vitae yenye mawasiliano na wadhamini 3.

  4. Kuambatisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa.

  5. Testimonial, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips hazitakubaliwa.

  6. Wenye tofauti ya majina waambatishe DEED POLL.

  7. Waombaji wa kada ya Dereva waambatishe vyeti vya mafunzo ya Udereva.

  8. Kuambatisha picha mbili (passport size) za hivi karibuni.

  9. Vyeti vya waliosoma nje vihakikiwe na TCU, NECTA au NACTE.

  10. Waliofukuzwa au kustaafishwa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali.

  11. Waajiriwa wa Umma walioko kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.

  12. Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.

  13. Mwisho wa kutuma maombi: 01 Julai 2025.

  14. Barua ya maombi iandikwe kwa:

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,
S.L.P 42, SINGIDA.

  1. Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia: https://portal.ajira.go.tz

Imetolewa na:
Kastori Msigala
MKURUGENZI MTENDAJI – HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI

TANGAZO LA AJIRA IKUNGI DC.pdf

Makala Nyingine:

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.