Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri Ya Wilaya Ya Bunda Juni, 2025

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA 13-06-2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda anawatangazia waombaji wa kazi kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 19 Juni 2025 hadi 23 Juni 2025 katika Shule ya Sekondari Mwibara, Kata ya Kibara.

Maelekezo Muhimu kwa Wasailiwa:

  1. Fika na barakoa (mask).

  2. Kuwa na kitambulisho halali (NIDA, mpiga kura, kazi, uraia au hati ya kusafiria).

  3. Leta vyeti halisi (cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, stashahada, shahada nk).

  4. Testimonials, statement of results na provisional results hazitakubaliwa.

  5. Gharama za chakula, usafiri na malazi ni za msailiwa mwenyewe.

  6. Kwa waliohitimu nje ya Tanzania, hakikisha vyeti vimeidhinishwa na TCU, NACTE au NECTA.

  7. Kwa kada zinazohitaji usajili wa kitaaluma, lete cheti cha usajili na leseni ya kazi.

  8. Ingia kwenye akaunti yako ya ajira.go.tz ili kunakili namba ya mtihani.

  9. Majina yanayotofautiana kwenye vyeti, lete deed poll iliyoidhinishwa.

  10. Madereva wa daraja E au C, leteni vyeti vya mafunzo ya udereva.

RATIBA YA USAILI:

DEREVA DARAJA II

  • Mchujo: 19-06-2025, 07:00 AM

  • Vitendo: 20-06-2025, 07:00 AM

  • Mahojiano: 21-06-2025, 07:00 AM

  • Mahali: Shule ya Sekondari Mwibara, Kata ya Kibara

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II

  • Mchujo: 22-06-2025, 07:00 AM

  • Mahojiano: 23-06-2025, 07:00 AM

  • Mahali: Shule ya Sekondari Mwibara, Kata ya Kibara

MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMII DARAJA LA II

  • Mchujo: 22-06-2025, 07:00 AM

  • Mahojiano: 23-06-2025, 07:00 AM

  • Mahali: Shule ya Sekondari Mwibara, Kata ya Kibara

MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II

  • Vitendo: 20-06-2025, 07:00 AM

  • Mahojiano: 21-06-2025, 07:00 AM

  • Mahali: Shule ya Sekondari Mwibara, Kata ya Kibara

Tangazo limetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

call_for_interview_advert (1) (2) pdf USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA.

Makala Nyingine: