Nafasi za Kazi Wauguzi 300 kwenda Saudi Arabia 2026 (ajira za uuguzi)

Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano kwa kushirikiana na Kampuni ya Dalba Consulting Group, imetangaza fursa kubwa ya ajira ya nafasi mia tatu ( 300 ) kwa Wauguzi Watanzania ambao watakwenda kufanya kazi katika Wizara ya Afya ya Nchini Saudi Arabia.

Kipaumbele kitatolewa kwa Waombaji Wanawake ambapo vigezo ni Waombaji wanatakiwa kuwa na umri kati ya miaka 23 hadi 45, wakiwa na Shahada ya kwanza au zaidi katika fani ya Uuguzi ambapo ni lazima kila Mwombaji awe na leseni hai kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC), pamoja na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili katika Sekta ya Uuguzi.

Wauguzi watakaopata ajira hii watajipatia mshahara wa kati ya shilingi milioni 3 hadi milioni 7 kwa mwezi ambapo mbali na mshahara huo Mwajiri atagharamia kikamilifu huduma za matibabu kwa kipindi chote cha ajira, Mwajiri atabeba gharama zote muhimu za maisha za Mwajiriwa ikiwa ni pamoja na tiketi ya Ndege ya kwenda na kurudi, malazi bora pamoja na chakula, pia usafiri kutoka Nyumbani hadi kituo cha kazi utagharamiwa kikamilifu.

Jinsi Ya Kutuma Maombi Ajira Mpya za Uuguzi(wauguzi) kwenda Saudi Arabia

Ajira hizi zitatolewa kwa mfumo wa mkataba wa miaka miwili ambao unaweza kuhuishwa kulingana na utendaji kazi na makubaliano ya pande husika, Waombaji wanatakiwa kutuma wasifu binafsi (CV) kwenda dalbatanzania@gmail.com, au kuwasiliana kupitia namba 0765070010 na 0744430010 kwa maelezo zaidi,

inasisitizwa kuwa ni muhimu kujisajili kupitia tovuti ya ajira ya Serikali https://jobs.kazi.go.tz baada ya kutuma maombi, mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 12 Aprili 2026.