Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Moshi Juni, 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi anawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kuomba nafasi za ajira zilizopo kama ilivyoainishwa hapa chini, kufuatia kibali cha ajira mpya Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 5
1.1 Majukumu ya Kazi
-
Kuorodhesha barua zinazoingia na zinazotoka.
-
Kusambaza na kurudisha majalada kwa watendaji.
-
Kutafuta na kurudisha nyaraka mahali pa kuhifadhi.
-
Kufuatilia mzunguko wa majalada (File Tracking).
-
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa.
1.2 Sifa za Mwombaji
-
Awe na elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).
-
Awe amehitimu Stashahada (Diploma – NTA level 6) katika fani ya Masijala kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
-
Awe na ujuzi wa kompyuta.
1.3 Mshahara
-
Kwa mujibu wa ngazi ya mishahara ya Serikali TGS C.
2.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 5
2.1 Majukumu ya Kazi
-
Kukagua gari kabla na baada ya safari.
-
Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali.
-
Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
-
Kukusanya na kusambaza nyaraka.
-
Kutunza taarifa za safari.
-
Kufanya usafi wa gari.
-
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa.
2.2 Sifa za Mwombaji
-
Awe na cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
-
Awe na Leseni ya Daraja E au C, akiwa ameendesha kwa angalau mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
-
Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
2.3 Mshahara
-
Kwa mujibu wa ngazi ya mishahara ya Serikali TGS B.
3.0 Masharti ya Jumla kwa Waombaji
-
Waombaji wote wawe raia wa Tanzania, wenye umri wa miaka 18 hadi 45 (isipokuwa walioko kazini Serikalini).
-
Wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba, waeleze aina ya ulemavu wao.
-
Dereva lazima aambatishe vyeti vya mafunzo ya udereva.
-
Kuambatisha Curriculum Vitae yenye maelezo ya mawasiliano na majina ya wadhamini watatu.
-
Waajiriwa wa umma walioko katika nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.
-
Kuambatisha vyeti halisi vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na mwanasheria au wakili.
-
Hakuna Testimonial, Provisional Results, Statement of Results au Result Slips zitakazokubalika.
-
Vyeti vya waliosoma nje vihakikiwe na TCU, NECTA au NACTE.
-
Waliofukuzwa au kustaafishwa katika utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali.
-
Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
-
Mwisho wa kupokea maombi: 29 Juni 2025.
-
Barua ya maombi iandikwe kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI,
S.L.P 3003, MOSHI.
-
Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa Recruitment Portal: https://portal.ajira.go.tz
Imetolewa na:
Shadrack M. Mhagama
MKURUGENZI MTENDAJI (W), MOSHI.
Makala Nyingine: