Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Kongwa Juni, 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kujaza nafasi za ajira mpya baada ya kupokea kibali cha ajira Kumb. Na. FA.87/97/01/99 cha tarehe 15 Mei 2025 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4
1.1 Majukumu ya Kazi
-
Kuorodhesha barua zinazoingia na zinazotoka.
-
Kusambaza na kurudisha majalada kwa watendaji.
-
Kutafuta na kurudisha nyaraka sehemu husika.
-
Kufuatilia mzunguko wa majalada (File Tracking).
1.2 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).
-
Stashahada (Diploma – NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
-
Awe na ujuzi wa kompyuta.
1.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS C.
2.0 Masharti ya Jumla kwa Waombaji
-
Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
-
Wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na waeleze aina ya ulemavu kwenye mfumo.
-
Kuambatisha Curriculum Vitae yenye maelezo ya mawasiliano na wadhamini 3.
-
Kuambatisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na mwanasheria au wakili.
-
Testimonial, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips hazitakubaliwa.
-
Vyeti vya waliosoma nje vihakikiwe na TCU, NECTA au NACTE.
-
Waliofukuzwa au kustaafishwa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali.
-
Waajiriwa wa Umma walioko kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.
-
Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
-
Mwisho wa kutuma maombi: 26 Juni 2025.
-
Barua ya maombi iandikwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa,
S.L.P 57, KONGWA.
-
Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia: https://portal.ajira.go.tz
Imetolewa na:
Dr. Omary A. Nkullo
MKURUGENZI MTENDAJI (W) – KONGWA
Makala Nyingine:
Tags: Wilaya Ya Kongwa