Majina ya walioitwa Usaili Tume ya Utumishi wa Mahakama Disemba 10, 2025 PDF nzima nimekuwekea hapo chini soma na unaweza kuipakua pia. Kuitwa kwenye usaili.
Kufuatia tangazo la nafasi za ajira mpya zilizotangazwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama tarehe 17 Novemba, 2025, napenda kuwafahamisha waombaji wa nafasi za kazi kwa kada mbalimbali kuwa, baada ya uchambuzi wa kina waombaji waliochaguliwa kuingia kwenye usaili wa hatua ya kwanza, watasailiwa kwa nafasi hizo kwa tarehe, muda na vituo vilivyooneshwa kwenye orodha ya majina ya wasailiwa iliyoambatishwa na Tangazo hili.

Hatua hii ya usaili itafanyika kwa njia ya Kielektroniki kwa kila Kada iliyoainishwa kwenye jedwali na tarehe husika kuanzia saa 2:30 asubuhi. Wasailiwa wote wafike na vyeti vyao halisi vya Elimu, Taaluma, kuzaliwa na kitambulisho chenye picha kinachotambulika na Serikali. Wasailiwa watakaofika kwenye vituo vya usaili bila kuwa na nyaraka zilizoainishwa ama kufika nje ya muda wa usaili uliopangwa hawatasailiwa. Wasailiwa wazingatie kuhudhuria usaili kwenye vituo walivyopangiwa.
Aidha, watakaofaulu usaili katika hatua ya kwanza watafahamishwa tarehe ya hatua nyingine ya usaili wa kujieleza (Oral Interview) na au vitendo (Practical interview) kupitia tovuti ya Tume ya Utumishi wa Mahakama www.jsc.go.tz Kwa taarifa hii, wote walioomba nafasi za ajira watembelee Tovuti ya Tume ili kuona kituo cha kufanyia usaili na muda uliopangwa.
Kwa wale ambao hawataona majina yao, watambue kuwa hawakupata nafasi ya kufanya usaili. Kwa maulizo zaidi piga; simu Na 0734219821 au 0738247341 na Barua pepe: maulizo.ajira@jsc.go.tz.
PDF ya Majina walioitwa Usaili Tume ya Utumishi wa Mahakama
TANGAZO-LA-KUITWA-KWENYE-USAILI-JSC_elimuforum.com
Makala Nyingine Zaidi:
Mfumo wa Maombi ya Ajira wa Tume ya Utumishi wa Mahakama JSC








Tuachie Maoni Yako