HESLB inakusanya Maoni kuhusu Huduma zao (bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini Tanzania imeanza rasmi kukusanya taarifa za maoni kuhusu huduma zao.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeanzisha tafiti tatu kupitia kitengo chake cha Mipango na Utafiti kwa lengo la kukusanya maoni ya wateja na wadau mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa. Tafiti hizi zinalenga kuboresha huduma kwa kuzingatia mapendekezo ya wadau. Tunakuomba ushiriki kwa kutoa maoni yako kupitia viunganishi vilivyopo kwenye mtandao.
Tafiti Zinazofanywa
- CUSTOMER EFFORT ONLINE LINK (CES)
Tafiti hii inalenga kutathmini jinsi ilivyo rahisi au vigumu kwa wateja wetu kupata huduma mbalimbali za HESLB. Tunaomba uwakilishe maoni yako kwa kufungua kiungo hiki:
CUSTOMER EFFORT ONLINE LINK (CES) - STAKEHOLDERS SATISFACTION (SSAT)
Tafiti hii inalenga kupima kiwango cha kuridhika kwa wadau wa HESLB kuhusu huduma zinazotolewa. Tafadhali shiriki kwenye utafiti huu kupitia kiungo hiki:
STAKEHOLDERS SATISFACTION (SSAT) - IMPACT OF LOANS ON HIGHER EDUCATION ACCESSIBILITY
Utafiti huu unaangazia athari za mikopo katika upatikanaji wa elimu ya juu. Kwa kushiriki, tembelea kiungo hiki:
IMPACT OF LOANS ON HIGHER EDUCATION ACCESSIBILITY
Watu Wanaohitajika Kujaza Tafiti Hizi
Maoni haya yanatakiwa kutolewa na makundi yafuatayo:
- Wanufaika wa Mikopo waliohitimu masomo.
- Waajiri wenye wanufaika wa mikopo ambao wanarejesha mikopo kupitia Employer Portal (EPO).
- Wanufaika wa Mikopo wanaoendelea na masomo.
- MDAs (Mamlaka za Serikali) – Hasa kwa ajili ya utafiti wa Kuridhika kwa Wadau (SSAT).
- Watoa Huduma – Hasa kwa utafiti wa Kuridhika kwa Wadau (SSAT).
- Wasionufaika na Mikopo (Umma).
NB: Ushiriki wako ni muhimu ili kuboresha huduma za HESLB kwa wateja na wadau wote. Tunakushukuru kwa kushiriki!
Makala Nyingine;
Huruma zenu ni nzuri na Bora Sana ila changamoto ni pale MA Ina return bila uzembe wa mwanafunzi lakini kuenda kumuomba inachukua muda sana kupata
Huduma zenu ni nzuri na Bora Sana ila changamoto ni pale MA Ina return bila uzembe wa mwanafunzi lakini kuenda kumuomba inachukua muda sana kupata