Wanafunzi 9,068 Waliopata mkopo awamu ya nne 2024/2025 pia utajifunza Jinsi Ya Kuangalia majina ya waliopata mkopo kwa awamu ya nne kupitia HESLB (Higher Education Students’ Loans Board) Bodi ya mikopo ya elimu ya juu Tanzania.
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) nchini Tanzania imeendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, ambapo awamu ya nne ya mgao wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2024/2025 imetangazwa. Katika awamu hii, jumla ya wanafunzi 9,068 wa shahada ya awali (Bachelor Degrees) na stashahada (Diploma) wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 27.52 bilioni.
Maelezo ya Mikopo ya Awamu ya Nne
Wanafunzi wa Shahada ya Awali
Wanafunzi wapya 4,400 wa mwaka wa kwanza waliodahiliwa katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini wamepangiwa mikopo ya jumla ya TZS 13.74 bilioni. Vilevile, wanafunzi wanaoendelea na masomo 2,646 wa shahada ya awali, wamepangiwa mikopo kwa mara ya kwanza (first-time continuing), yenye thamani ya TZS 8.37 bilioni.
Mikopo kwa Stashahada
Katika awamu hii, kuna pia wanafunzi wapya 2,022 wa stashahada wa mwaka wa kwanza ambao wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 5.41 bilioni. Wanafunzi hawa wamedahiliwa katika programu za kipaumbele katika vyuo vya kati nchini Tanzania.
Ruzuku ya ‘Samia Scholarship’
Mpaka sasa, kiasi cha TZS 3.14 bilioni zimetolewa kama ruzuku kwa wanafunzi 625 wanaonufaika na ‘Samia Scholarship’ katika fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati, na Tiba kwa mwaka wa masomo 2024/2025. Ruzuku hii imetolewa kwa wanafunzi 588 wa awamu ya kwanza, 11 wa awamu ya pili, na 26 wa awamu ya tatu.
Kufunguliwa kwa Dirisha la Rufaa 2024/2025
Wanafunzi ambao hawakuridhika na viwango vya mikopo walivyopangiwa au ambao hawakupata mikopo kabisa wanaweza kukata rufaa. Dirisha la rufaa litafunguliwa kuanzia Jumatatu, Novemba 4 hadi Jumapili, Novemba 10, 2024.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliopata Mkopo kwa Awamu ya Nne
Ili kuangalia majina ya waliopata mkopo kwa awamu ya nne kupitia mfumo wa OLAMS wa HESLB, fuata hatua hizi:
- Tembelea tovuti ya HESLB kwenye mfumo wa OLAMS: https://olas.heslb.go.tz/olams/account/login.
- Ingia kwa kutumia taarifa zako binafsi ili kuona kama umepangiwa mkopo katika awamu ya nne.
Kwa taarifa zaidi na msaada, wanafunzi wanaweza kufika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) au kutembelea tovuti yao rasmi.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
DAR ES SALAAM
Jumanne, Oktoba 29, 2024
Makala Nyingine:
Leave a Reply