Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Muheza Juni, 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za ajira mpya baada ya kupokea kibali cha ajira Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili 2025 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 5
1.1 Majukumu ya Kazi
-
Kuchapa barua, taarifa na nyaraka mbalimbali.
-
Kupokea wageni na kushughulikia mahitaji yao.
-
Kutunza kumbukumbu za matukio, vikao, safari na ratiba mbalimbali.
-
Kutafuta na kusambaza nyaraka kwa maofisa husika.
-
Kupanga dondoo na maandalizi ya vikao mbalimbali.
-
Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
-
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi.
1.2 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).
-
Stashahada (Diploma) au NTA Level 6 ya Uhazili.
-
Kuwa amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja.
-
Awe na ujuzi wa programu za kompyuta za ofisi (Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail, Publisher).
1.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS C.
2.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 6
2.1 Majukumu ya Kazi
-
Kukagua gari kabla na baada ya safari.
-
Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi.
-
Kufanya matengenezo madogo ya gari.
-
Kukusanya na kusambaza nyaraka.
-
Kutunza taarifa za safari kwenye daftari la safari.
-
Kufanya usafi wa gari.
-
Kufanya kazi nyingine kwa maelekezo ya msimamizi.
2.2 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).
-
Leseni ya Daraja E au C; ameendesha kwa mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
-
Cheti cha mafunzo ya msingi ya Udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
2.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS B.
3.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4
3.1 Majukumu ya Kazi
-
Kuorodhesha barua zinazoingia na zinazotoka.
-
Kusambaza na kurudisha majalada kwa watendaji.
-
Kutafuta na kurudisha nyaraka sehemu husika.
-
Kufuatilia mzunguko wa majalada (File Tracking).
3.2 Sifa za Mwombaji
-
Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).
-
Stashahada (Diploma – NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
-
Awe na ujuzi wa kompyuta.
3.3 Mshahara
-
Ngazi ya mshahara TGS C.
4.0 Masharti ya Jumla kwa Waombaji
-
Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
-
Kuambatisha cheti cha kuzaliwa.
-
Kuambatisha Curriculum Vitae yenye mawasiliano na wadhamini 3.
-
Kuambatisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa.
-
Testimonial, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips hazitakubaliwa.
-
Dereva II waambatishe vyeti vya mafunzo ya Udereva.
-
Kuambatisha picha mbili (passport size) za hivi karibuni.
-
Vyeti vya waliosoma nje vihakikiwe na TCU, NECTA au NACTE.
-
Waliofukuzwa au kustaafishwa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali.
-
Waajiriwa wa Umma walioko kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.
-
Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
-
Mwisho wa kutuma maombi: 01 Julai 2025.
-
Barua ya maombi iandikwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza,
S.L.P 20, MUHEZA.
-
Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia: https://portal.ajira.go.tz
Imetolewa na:
Dr. Jumaa M. Mhina
MKURUGENZI MTENDAJI – HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA
Makala Nyingine:
Tags: Wilaya Ya Muheza