Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Sikonge Juni, 2025

Filed in Ajira by on June 21, 2025 0 Comments

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za ajira mpya baada ya kupokea kibali Kumb. Na. FA.97/288/01/25 cha tarehe 29 Aprili 2025 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

1.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4

1.1 Majukumu ya Kazi

  • Kuorodhesha barua zinazoingia na zinazotoka.

  • Kusambaza na kurudisha majalada kwa watendaji.

  • Kutafuta na kurudisha nyaraka sehemu husika.

  • Kufuatilia mzunguko wa majalada (File Tracking).

  • Kufanya kazi nyingine kwa maelekezo ya msimamizi wake.

1.2 Sifa za Mwombaji

  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).

  • Stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

  • Awe na ujuzi wa kompyuta.

1.3 Mshahara

  • Ngazi ya mshahara TGS C.

2.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 4

2.1 Majukumu ya Kazi

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka mbalimbali.

  • Kupokea wageni na kuwaelekeza sehemu sahihi.

  • Kutunza kumbukumbu za matukio, vikao, safari na miadi.

  • Kutafuta na kusambaza nyaraka kwa maofisa husika.

  • Kupanga dondoo na maandalizi ya vikao mbalimbali.

  • Kuandaa orodha ya vifaa vya ofisi.

2.2 Sifa za Mwombaji

  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).

  • Stashahada (Diploma) au NTA Level 6 ya Uhazili.

  • Kuwa amefaulu Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja.

  • Ujuzi wa programu za kompyuta za ofisi (Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail, Publisher).

2.3 Mshahara

  • Ngazi ya mshahara TGS C.

3.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 5

3.1 Majukumu ya Kazi

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari.

  • Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi.

  • Kufanya matengenezo madogo ya gari.

  • Kutunza na kuandika taarifa za safari (log book).

  • Kukusanya na kusambaza nyaraka.

  • Kufanya usafi wa gari.

  • Kufanya kazi nyingine kadri ya maelekezo ya msimamizi.

3.2 Sifa za Mwombaji

  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).

  • Leseni ya Daraja E au C; awe ameendesha kwa mwaka mmoja bila kusababisha ajali.

  • Cheti cha mafunzo ya msingi ya Udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.

3.3 Mshahara

  • Ngazi ya mshahara TGS B.

4.0 Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  1. Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.

  2. Wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na waeleze aina ya ulemavu kwenye mfumo.

  3. Kuambatisha Curriculum Vitae yenye maelezo ya mawasiliano na wadhamini 3.

  4. Kuambatisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na mwanasheria au wakili.

  5. Testimonial, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips hazitakubaliwa.

  6. Waajiriwa wa umma walio na sifa mpya wapitishe maombi yao kwa waajiri wao.

  7. Vyeti vya waliosoma nje vihakikiwe na TCU, NECTA au NACTE.

  8. Waliofukuzwa au kustaafishwa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali.

  9. Waajiriwa wa Umma walioko kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.

  10. Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.

  11. Dereva II waambatishe vyeti vya mafunzo ya Udereva.

  12. Tofauti ya majina lazima iambatishwe na DEED POLL.

  13. Mwisho wa kutuma maombi: 29 Juni 2025.

  14. Barua ya maombi iandikwe kwa:

MKURUGENZI MTENDAJI (W),
S.L.P 70, SIKONGE.

  1. Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia: https://portal.ajira.go.tz

Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI (W) – SIKONGE

TANGAZO LA KAZI SIKONGE.pdf

Makala Nyingine:

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.