Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Mji Masasi Juni, 2025

Filed in Ajira by on June 21, 2025 0 Comments

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa stahiki kujaza nafasi za ajira mpya baada ya kupokea kibali Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili 2025 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

1.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 5

1.1 Majukumu ya Kazi

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari.

  • Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi.

  • Kufanya matengenezo madogo ya gari.

  • Kukusanya na kusambaza nyaraka.

  • Kutunza taarifa za safari kwenye daftari la safari.

  • Kufanya usafi wa gari.

  • Kufanya kazi nyingine zitakazopangwa na msimamizi au mwajiri.

1.2 Sifa za Mwombaji

  • Awe na cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).

  • Awe na leseni ya Daraja E au C, na awe ameendesha kwa mwaka mmoja bila kusababisha ajali.

  • Awe na cheti cha mafunzo ya msingi ya Udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.

1.3 Mshahara

  • Ngazi ya mshahara TGS B1.“`

2.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 5

2.1 Majukumu ya Kazi

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka mbalimbali.

  • Kupokea wageni na kushughulikia mahitaji yao.

  • Kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, vikao, na ratiba za kazi.

  • Kutafuta na kusambaza majalada na nyaraka kwa maofisa husika.

  • Kuandaa dondoo na maandalizi ya vikao mbalimbali.

  • Kuandaa orodha ya vifaa vya ofisi.

2.2 Sifa za Mwombaji

  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).

  • Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili.

  • Kuwa amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja.

  • Awe na ujuzi wa programu za kompyuta za ofisi (Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail, Publisher).

2.3 Mshahara

  • Ngazi ya mshahara TGS C1.

3.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4

3.1 Majukumu ya Kazi

  • Kuorodhesha barua zinazoingia na zinazotoka.

  • Kusambaza na kurudisha majalada kwa watendaji.

  • Kutafuta na kurudisha nyaraka sehemu husika.

  • Kufuatilia mzunguko wa majalada (File Tracking).

3.2 Sifa za Mwombaji

  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).

  • Stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

  • Ujuzi wa kompyuta.

3.3 Mshahara

  • Ngazi ya mshahara TGS C1.

4.0 Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  1. Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.

  2. Kuambatisha Cheti cha Kuzaliwa.

  3. Kuambatisha maelezo binafsi (Detailed CV) yenye mawasiliano na wadhamini 3.

  4. Kuambatisha vyeti vya elimu na taaluma kwa mujibu wa sifa za kazi husika.

  5. Testimonial, Provisional Results, Statement of Results na Result Slips hazitakubaliwa.

  6. Dereva II waambatishe vyeti vya mafunzo ya udereva.

  7. Kuambatisha picha mbili (passport size) za hivi karibuni.

  8. Waliosoma nje wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU, NECTA au NACTE.

  9. Waliofukuzwa au kustaafishwa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali.

  10. Waajiriwa wa Umma walioko kwenye nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.

  11. Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.

  12. Mwisho wa kutuma maombi: 29 Juni 2025.

  13. Barua ya maombi iandikwe kwa:

Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji Masasi,
S.L.P 447, MASASI.

  1. Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kupitia: https://portal.ajira.go.tz

Imetolewa na:
Reuben S. Jichabu
MKURUGENZI WA MJI – MASASI

TANGAZO LA KAZI MASASI TC.pdf

Makala Nyingine:

Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Ngorongoro Juni, 2025

Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Moshi Juni, 2025

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.