Yanga Watangaza Kocha Mpya 2025 Miloud Hamdi

Klabu ya Yanga Watangaza Kocha Mpya 2025 Miloud Hamdi, Uongozi wa Klabu ya Young Africans SC umefikia makubaliano ya pande mbili kuvunja mkataba na Kocha Sead Ramovic na msaidizi wake Mustafa Kodro.

Katika hatua nyingine, Klabu ya Young Africans SC inamtangaza Kocha wake mpya, Miloud Hamdi mwenye uraia wa Algeria na Ufaransa.

Unaweza Kusoma: Ratiba ya Mechi za Yanga Ligi Kuu NBC 2024/2025

Kocha Hamdi mwenye uzoefu mkubwa wa kufundisha soka akiwa amefanya kazi barani Ulaya, Asia na Afrika, anaungana na timu mara moja kuanza majukumu yake mapya.

Kocha huyo mbali na uzoefu alionao, pia ana mafanikio makubwa katika soka la Afrika akishinda taji la Ligi Kuu ya Algeria na kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2015-2016 akiwa na USM Alger.

Imetolewa na

Idara ya habari na mawasiliano
Young Africans Sports Club.

Makala Nyingine: