Waliochaguliwa kidato cha kwanza 2026 (Wanafunzi 937,581) Form one Selection 2025/2026, Jumla ya wanafunzi 937,581 sawa na asilimia 100 ya wanafunzi wote waliokidhi vigezo wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza kwa mwaka wa masomo 2026.
Uchaguzi huu unahusisha wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) mwaka 2025 na kupata alama kati ya 121 hadi 300 Shule Walizopangiwa Darasa la Saba 2026.
Taarifa hizi zimetolewa leo Desemba 4, 2025 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Sifa za Wanafunzi Waliochaguliwa
Kwa mujibu wa Profesa Shemdoe, uchaguzi wa wanafunzi umefanyika kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kila mwanafunzi aliyepata jumla ya alama kati ya 121 hadi 300 amepangiwa shule ya sekondari ya Serikali.
Takwimu za Ujumla za Wanafunzi Waliochaguliwa
| Kundi la Wanafunzi | Idadi |
|---|---|
| Jumla ya Wanafunzi Wote | 937,581 |
| Wasichana | 508,477 |
| Wavulana | 429,104 |
| Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum | 3,228 |
| Wasichana wenye Mahitaji Maalum | 1,544 |
| Wavulana wenye Mahitaji Maalum | 1,684 |
| Jumla ya Shule za Sekondari za Serikali | 5,230 |
Wanafunzi wote hao wamepangiwa shule za sekondari za Serikali kwa ajili ya kuanza masomo ya Kidato cha Kwanza mwaka 2026.
Wanafunzi Waliopangiwa Shule za Ufaulu wa Juu
Wanafunzi 815 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari zinazopokea wanafunzi wenye ufaulu wa juu.
| Aina ya Wanafunzi | Idadi |
|---|---|
| Jumla | 815 |
| Wasichana | 335 |
| Wavulana | 480 |
Baadhi ya shule hizo ni:
- Ilboru Secondary School
- Msalato Secondary School
- Kibaha Secondary School
- Kilakala Secondary School
- Mzumbe Secondary School
- Tabora Boys
- Tabora Girls
Wanafunzi wa Shule za Amali za Bweni
Wanafunzi 3,411 wamechaguliwa kujiunga na shule za amali za bweni.
| Aina ya Wanafunzi | Idadi |
|---|---|
| Jumla | 3,411 |
| Wasichana | 1,279 |
| Wavulana | 2,162 |
Wanafunzi wa Shule za Bweni za Kitaifa
Jumla ya wanafunzi 7,360 wamechaguliwa kujiunga na shule za bweni za kitaifa.
| Aina ya Wanafunzi | Idadi |
|---|---|
| Jumla | 7,360 |
| Wasichana | 5,014 |
| Wavulana | 2,346 |
Wanafunzi wa Shule za Sekondari za Kutwa
Wanafunzi wengi wamepangiwa shule za sekondari za kutwa zilizopo karibu na walikosoma elimu ya msingi.
| Aina ya Wanafunzi | Idadi |
|---|---|
| Jumla | 925,065 |
| Wasichana | 501,849 |
| Wavulana | 424,116 |
Kuanza kwa Masomo Kidato cha Kwanza 2026
Serikali imefanya maandalizi ya mapema kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanajiunga na elimu ya sekondari kwa wakati. Muhula wa kwanza wa masomo kwa Kidato cha Kwanza utaanza rasmi tarehe 13 Januari, 2026.
Ushauri kwa Wanafunzi na Wazazi
Profesa Shemdoe amewataka wanafunzi kutumia vizuri fursa waliyoipata kwa kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao binafsi na matarajio ya wazazi wao. Aidha, amewahimiza wazazi na walezi kufanya maandalizi ya kutosha kwa watoto wao ili kuhakikisha wanaripoti shuleni kwa wakati.
Maelekezo kwa Mikoa na Halmashauri
Mikoa na Halmashauri zote nchini zimeelekezwa kuhakikisha:
- Wanafunzi wote waliochaguliwa wanaripoti shuleni.
- Wanafunzi wanaandikishwa kwa wakati.
- Mazingira wezeshi ya utekelezaji wa mitaala mipya yanaimarishwa.
- Shule zinatumia vyema kipindi cha maandalizi (orientation) kuwajengea wanafunzi uwezo wa mawasiliano ya lugha ya Kiingereza na kuwasaidia kuchagua fani wanazopenda.
Uchaguzi wa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza 2026 umefanyika kwa mafanikio makubwa, ukihusisha wanafunzi wote 937,581 waliokuwa na sifa.
Serikali, wazazi, walezi na wadau wa elimu wanapaswa kushirikiana kuhakikisha wanafunzi wote wanaanza masomo Januari 2026 bila vikwazo na kubaki shuleni hadi kukamilisha elimu ya sekondari.
Tazama Hapa Form one selection 2026 au https://selection.tamisemi.go.tz/
WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA – 2026, KULINGANA NA MATOKEO YALIYOTANGAZWA NA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA (NECTA)
BOFYA JINA LA SHULE KUONA ORODHA YA WANAFUNZI
https://selection.tamisemi.go.tz/allocations/2025/first-selection/index.html
Makala Zinazoendana:
Shule walizopangiwa darasa la saba 2025/2026 TAMISEMI








Tuachie Maoni Yako