Simba Yatangaza haitocheza Mechi Ya Derby Tar 8, Machi 2025, Ni baada ya kufanyiwa vuruu jana wakijiandaa kungia taifa ili kufanya mazoezi yao ya mwisho kabla ya mechi yao dhidi ya Yanga.
Klabu ya Simba imesema imesikitishwa na vitendo visivyo vya kiungwana dhidi ya Timu hiyo kuelekea Mchezo wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Yanga, Simba ikiwa timu mgeni ambapo kufuatia suala hilo Simba imesema haitoshiriki mchezo husika.
Taarifa iliyotolewa na Menejimenti ya Simba imesema kwa mujibu wa kanuni 17 (45) ya Kanuni za Ligi Kuu Bara, Timu Mgeni ina haki ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi angalau mara moja kabla ya siku ya mechi katika muda tarajiwa wa mchezo husika”
“Kwa makusudi Simba imenyimwa haki hiyo licha ya kufika uwanjani katika muda husika, katika sintofahamu hiyo, Simba iliarifiwa na Meneja wa Uwanja kuwa hana maelekezo ya kuruhusu mazoezi kufanyika bila maelekezo ya kamishna wa Mchezo, pamoja na Kamishna wa mchezo husika kufika, Mabaunsa wa Klabu ya Yanga walivamia msafara wa Simba huku wakiendelea na vurugu na wakizua Msafara wa simba kuingia uwanjani kufanya mazoezi”
“Jitihada za Simba kupata ufumbuzi wa changamoto hiyo hazikuzaa matunda kwa zaidi ya masaa mawili kabla ya Simba kuondoka eneo la nje ya uwanja kwa sababu za kiusalama ambazo zimerekodiwa kwa ajili ya ushahidi, kufuatia ukiukwaji huo wa taratibu za mchezo, Simba haitoshiriki mchezo husika na haki zote zimehifadhiwa, Simba inahimiza kuchukuliwa kwa hatua stahiki dhidi ya Wahusika wote wa sakata hili”
🚨 TAARIFA KWA UMMA. #WenyeNchi #NguvuMoja
Makala Nyingine:
Leave a Reply