Ratiba ya Yanga Klabu Bingwa 2025/2026 CAF champions league

Young Africans SC (Yanga) walishiriki kwenye CAF Champions League 2025/2026 kama mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC. Timu ya Wananchi ilifanya vizuri kwenye hatua za awali, lakini ilishindwa kuendelea baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye kundi lao.

Hapa chini ni ratiba kamili pamoja na matokeo ya mechi zote za Yanga kwenye mashindano hayo.

1. Hatua ya Awali (Preliminary Round)

Yanga vs Wiliete de Benguela (Angola)

Mechi Tarehe Uwanja Matokeo
Mechi ya Kwanza 19 Septemba 2025 Away Wiliete 0-3 Yanga
Mechi ya Kurudi 27 Septemba 2025 Home Yanga 2-0 Wiliete

Jumla: Yanga 5-0 Wiliete Yanga waliendelea kwa ushindi mkubwa.

2. Round ya Kwanza (First Round)

Yanga vs Silver Strikers (Malawi)

Mechi Tarehe Uwanja Matokeo
Mechi ya Kwanza 18 Oktoba 2025 Away Silver Strikers 1-0 Yanga
Mechi ya Kurudi 25 Oktoba 2025 Home Yanga 2-0 Silver Strikers

Jumla: Yanga 2-1 Silver Strikers Yanga walirejesha hasara na kufuzu kwenye Group Stage.

3. Group Stage (Kundi B)

Yanga waliwekwa kwenye Kundi B pamoja na:

  • Al Ahly (Misri)
  • AS FAR Rabat (Morocco)
  • JS Kabylie (Algeria)

Ratiba na Matokeo ya Group Stage

Mechi Tarehe Uwanja Matokeo
1 22 Novemba 2025 Home (Amaan Stadium) Yanga 1-0 AS FAR
2 28 Novemba 2025 Away JS Kabylie 0-0 Yanga
3 23 Januari 2026 Away (Borg El Arab) Al Ahly 2-0 Yanga
4 31 Januari 2026 Home Yanga 1-1 Al Ahly
5 7 Februari 2026 Away AS FAR 1-0 Yanga
6 15 Februari 2026 Home Yanga 3-0 JS Kabylie

Jedwali la Mwisho la Kundi B

Nafasi Timu Mechi Pointi Gol zilizofunga Gol zilizofungwa
1 Al Ahly 6 10 8 3
2 AS FAR Rabat 6 9 3 2
3 Yanga SC 6 8 5 4
4 JS Kabylie 6 3 1 8

Yanga walimaliza na pointi 8 (ushindi 2, sare 2, kushindwa 2) na kushindwa kufuzu kwenye robo fainali.

Walifunga mechi yao ya mwisho kwa ushindi mkubwa wa 3-0 dhidi ya JS Kabylie, lakini matokeo ya mechi nyingine kwenye kundi yaliwafanya washindwe kuendelea.

Uchambuzi Mfupi

  • Yanga walicheza vizuri nyumbani (ushindi 2 na sare 1).
  • Walipata shida ugenini, hasa dhidi ya Al Ahly na AS FAR.
  • Walionyesha ubora wao kwa kuifunga JS Kabylie 3-0 katika mechi ya mwisho.

Ingawa hawakuendelea, Yanga walionyesha ushindani mkubwa kwenye kundi gumu lililokuwa na Al Ahly na AS FAR.

Makala Nyingine: