Ratiba Ya Mtihani wa darasa la saba 2025 PSLE

Ratiba Ya Mtihani wa darasa la saba 2025 PSLE exam timetable, Ratiba ya mtihani wa darasa la saba 2025 pdf,

RATIBA YA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PRIMARY SCHOOL LEAVING EXAMINATION TIMETABLE) SEPTEMBA, 2025

PDF Kamili Hapa: PSLE_TIMETABLE_2025

MAELEKEZO MUHIMU

  1. Hakikisha kuwa unayo Ratiba ya Mtihani ya mwaka 2025 iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
  2. Hakikisha kwamba unasoma jina la somo juu ya bahasha husika na kuthibitisha kuwa somo hilo ndilo linalostahili kufanyika wakati huo kulingana na Ratiba ya Mtihani.
  3. Kabla ya kufungua bahasha, mpe Mtahiniwa asome kwa sauti jina la somo lililoandikwa juu ya bahasha ili kuthibitisha ni somo husika kwa mujibu wa ratiba.
  4. Endapo utata utajitokeza kati ya maelekezo yaliyomo katika Karatasi ya Mtihani na Ratiba ya Mtihani, maelekezo yaliyomo katika karatasi ya Mtihani husika ndiyo yatakayofuatwa.
  5. Watahiniwa wenye mahitaji Maalum (Wasioona, Uoni hafifu, Viziwi) waongezewe MUDA WA ZIADA WA DAKIKA 20 KWA KILA SAA kwa somo la Hisabati na DAKIKA 10 KWA KILA SAA kwa masomo mengine.
  6. Watahiniwa wenye   UONI    HAFIFU    wapewe    karatasi                      za          Mtihani zenye       maandishi yaliyokuzwa, zilizoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania kwa matumizi yao.
  7. Watahiniwa waelekezwe;

Kuingia ndani ya chumba cha Mtihani nusu saa kabla ya muda wa Mtihani na watakaochelewa kwa zaidi ya nusu saa baada ya Mtihani kuanza hawataruhusiwa.

Kufuata maelekezo yote yatakayotolewa na wasimamizi wa Kuandika namba ya Mtihani kwa

Kutofanya mawasiliano ya maneno au kwa njia yoyote baina yao. Ikiwa Mtahiniwa ana tatizo anatakiwa kunyoosha mkono ili kuomba msaada kwa msimamizi wa Mtihani.

Kutojihusisha na   vitendo   vya   udanganyifu  katika mtihani kwani watakaojihusisha matokeo yao yatafutwa.

Makala Nyingine: