Posho na Mishahara ya Walimu wa Kujitolea 2025, Kupitia Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Mh. Deus Sangu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza rasmi kuwa kuanzia tarehe 01 Julai 2025, mwongozo mpya wa Walimu wa Kujitolea utaanza kutumika nchini kote.
Huu ni mpango wa kimkakati wa kuziba mapungufu ya watumishi katika sekta ya elimu, hasa maeneo yenye upungufu mkubwa wa walimu.
Kwa Nini Ujitolee Katika Taasisi za Serikali?
Tanzania inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wafanyakazi katika sekta muhimu kama elimu na afya. Ili kukabiliana na changamoto hii:
- Serikali imeanzisha nafasi rasmi za kazi za kujitolea.
- Walimu wa kujitolea watapewa mikataba maalumu yenye malipo ya kimsingi.
- Manufaa ya kujitolea ni pamoja na:
- Kupata uzoefu wa vitendo kazini,
- Kupokea msaada wa kifedha (posho),
- Kupata kipaumbele katika ajira za Serikali pindi nafasi zitakapopatikana.
Malipo Rasmi ya Walimu wa Kujitolea 2025
Serikali imetangaza viwango maalum vya malipo kwa walimu wa kujitolea kulingana na ngazi ya shule wanazofundisha. Malipo haya yatatolewa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri husika.
Aina ya Shule | Kiasi cha Malipo kwa Mwezi (Tsh) |
---|---|
Shule za Msingi | Kuanzia Tsh 250,000 |
Shule za Sekondari | Kuanzia Tsh 300,000 |
💡 Malipo haya yanaweza kutofautiana kidogo kutegemeana na uwezo wa kifedha wa halmashauri husika, lakini viwango hivi ni vya chini kabisa vinavyopaswa kulipwa.
Mpango huu wa walimu wa kujitolea siyo tu unasaidia kuziba pengo la walimu mashuleni, bali pia ni fursa muhimu kwa wahitimu wapya wa fani ya elimu kujijengea uzoefu na kujiweka karibu zaidi na ajira za Serikali.
Walimu wote wenye nia ya kujitolea wanahimizwa kufuatilia matangazo ya nafasi hizi katika halmashauri zao na kuhakikisha wanazingatia masharti ya mwongozo mpya utakaoanza Julai 2025.
Makala Nyingine:
Hongra serikali kwa kusikia kilio cha walumu wa kujitolea.Atleast hizo posho zitapunguza gharama za maisha kwa walimu wakujitolea.
Kabisaaa! Hongereni Sana Serikali kwa kuliona hilo maana daah walimu wa kujitolea tunapitia changamoto nyingi sana hususani za kiuchumi nawaombeni huo mwezi July na iwe kweli maana ni hatari sana ni mwaka wa tatu Sasa najitolea..
Binafsi mim nampongeza raisi wetu mama SHM anajitahidi kutoa ajira mbalimbali ikiwemo sekta ya ualimu. Tuendelee kumuunga mkono
Habari mku?
Naipongeza serikali yetu kw hatua hii na fursa hizi zitawezesha kuondoa uhaba waalimu na kulinda uwezo wa waalimu hao
Naipongeza sana serikali kwa kuwakumbuka walimu wa kujitolea. Ila imebezi sana kwa shule za msingi, lini watatoa na shule za sekondari ili nao waweze kuomba kujitolea.
Mbna posho ndogo Kwa usawa wa maisha ya sas hyo inaishia kweny Kodi tu hujala hujavaa
Mbona nasikia halmashauri zingine wameanza kulipa vipi jaman Kuna ukweli wowote?
Naomba tuwasiliane
0614111991
WhatsApp 0676111991