Habari njema, Nafasi za Mafunzo ya ufundi Stadi fani mbalimbali 2025/2026, Serikali yatangaza nafasi 8,000 za mafunzo ya ufundi stadi katika fani mbalimbali nchini.
Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inatekeleza Programu ya Kukuza Ujuzi nchini inayolenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira.
Mafunzo ya ufundi Stadi fani mbalimbali 2025
4. Maombi yawasilishwe kuanzia tarehe 30 Januari, 2025 hadi 12 Februari, 2025 yakiambatana na nyaraka zifuatazo:
- Barua ya maombi ya mafunzo;
- Nakala ya Cheti cha kuzaliwa;
- Nakala ya Cheti cha elimu uliyohitimu;
- Kitambulisho cha uraia / kadi ya mpiga kura (Kwa wenye miaka 18 na kuendelea);
- Barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji anakoishi mwombaji; na
- Picha nne za paspoti (ziandikwe majina matatu ya mwombaji kwa nyuma).
Sifa za kujiunga na mafunzo haya ni:
Elimu ya msingi au zaidi kwa fani za ubunifu wa mitindo na ushonaji nguo, ufundi bomba, ujenzi, useremala, uchomeleaji na uungaji vyuma, upakaji rangi na maandishi ya alama;
Elimu ya kidato cha nne na kuendelea kwa fani nyingine zilizobaki zikijumuisha fani ya utengenezaji wa vipuri vya mitambo, ufundi magari, umeme wa majumbani na viwandani, umeme wa magari na umeme wa jua (solar);
Awe Mtanzania;
Awe na umri kati ya miaka 15-35; na
Awe mwenye afya njema.
Vijana Wenye Ulemavu wanasisitizwa kuomba fursa hizi na watapewa kipaumbela katika nafasi za mafunzo haya;
Maombi yachukuliwe na kuwasilishwa kwenye vyuo vilivyo katika mkoa wako ambavyo vimekubaliwa na Serikali kutoa mafunzo haya.
Watakaokidhi vigezo na sifa tu ndio watakaochanguliwa
Tangazo hili linapatikana katika Tovuti ya Ofisi (www.kazi.go.tz)
Makala Nyingine:
Leave a Reply