Nafasi Za Kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama June, 2025
Nafasi Za Kazi Tume ya Utumishi wa Mahakama June, 2025, ajira mpya JSC Ajira portal registration Jsc Ajira portal login TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI – TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
Juni 03, 2025 – Dodoma.
Tume ya Utumishi wa Mahakama inatangaza nafasi za ajira mpya kwa Watanzania wenye sifa stahiki kuajiriwa katika Mahakama ya Tanzania. Fuatilia tangazo hili kwa nafasi, sifa na majukumu ya kila kada kama ifuatavyo:
1. Hakimu Mkazi II – TJS II
- Sifa: Shahada ya Sheria (LL.B) na Stashahada ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania). Wenye cheti cha kompyuta ni kipaumbele.
- Kazi: Kusikiliza mashauri ya jinai/madai/ndoa/mirathi, kutoa hukumu, kusuluhisha mashauri, kufanya tafiti za kisheria n.k.
2. Afisa Utumishi II – TGS D
- Sifa: Shahada ya Rasilimali Watu, Sociology, Utawala au Mipango ya Watumishi. Ujuzi wa kompyuta ni muhimu.
- Kazi: Kudhibiti kumbukumbu za watumishi, kutafsiri miundo ya ajira, kupanga mafunzo, kuchambua takwimu n.k.
3. Msaidizi wa Hesabu II – TGS B
- Sifa: Cheti cha Astashahada ya Uhasibu au ATEC I ya NBAA.
- Kazi: Kutunza kumbukumbu na nyaraka za hesabu, kuandika rejista, kupeleka nyaraka benki n.k.
4. Opereta wa Kompyuta II – TGS C
- Sifa: Stashahada ya Kompyuta na uzoefu wa miaka 3.
- Kazi: Kazi za kiufundi za TEHAMA, kutunza data na vitabu vya matumizi ya kila siku.
5. Opereta Msaidizi wa Kompyuta – TGS B
- Sifa: Astashahada ya mwaka mmoja ya masomo ya awali ya Kompyuta.
- Kazi: Kuingiza taarifa kwenye mifumo ya TEHAMA, kuchambua nakala, kutoa ripoti n.k.
6. Mkutubi II – TGS D
- Sifa: Shahada ya Ukutubi.
- Kazi: Kupanga kazi, kuelekeza wakutubi, kuhakikisha usafi wa maktaba n.k.
7. Msaidizi wa Maktaba II – TGS B
- Sifa: Cheti cha Kidato cha IV na mafunzo ya wasaidizi wa maktaba.
- Kazi: Kuandikisha wasomaji, kupanga vitabu, kukarabati vitabu n.k.
8. Mpishi – TGS C
- Sifa: Cheti cha Food Production na uzoefu wa miaka 3.
- Kazi: Kupika, kusafisha jiko, kutunza vyombo vya kupikia.
9. Msaidizi wa Kumbukumbu II – TGS C
- Sifa: Stashahada ya Utunzaji Kumbukumbu au Sheria, na ujuzi wa kompyuta.
- Kazi: Kutunza masjala na mafaili, kuandika samansi, kuandaa orodha ya kesi n.k.
10. Afisa Mwendesha Ofisi Daraja II – TGS D
- Sifa: Shahada ya Uhazili, hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza 120 wpm, ujuzi wa kompyuta.
- Kazi: Kuratibu shughuli za ofisi, kufuatilia maagizo, kuandaa vikao n.k.
11. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II – TGS C
- Sifa: Stashahada ya Uhazili, hatimkato ya 100 wpm, matumizi ya Word, Excel n.k.
- Kazi: Kuchapa barua, kupokea wageni, kutunza ratiba na kumbukumbu n.k.
12. Dereva II – TGS B
- Sifa: Kidato cha IV, Leseni Daraja E/C1, mafunzo ya VETA.
- Kazi: Kuendesha gari, kufanya ukaguzi na matengenezo madogo, kukusanya nyaraka.
13. Mlinzi – TGOS A
- Sifa: Kidato cha IV, cheti cha Mgambo au JKT.
- Kazi: Kulinda mali na majengo, kudhibiti wageni, kutoa ushauri wa usalama.
14. Msaidizi wa Ofisi – TGOS A
- Sifa: Kidato cha IV (Hisabati, Kiswahili, Kiingereza).
- Kazi: Usafi wa ofisi, kusambaza barua, kupika chai, kutayarisha majalada n.k.
Maelekezo Muhimu kwa Waombaji
- Muombaji awe Raia wa Tanzania, umri miaka 18–45, asiwe na kosa la jinai.
- Maombi yatumiwe kwa njia ya kielektroniki tu kupitia: www.jsc.go.tz
- Ambatanisha:
- Vyeti vya elimu na matokeo
- Cheti cha kuzaliwa
- Picha (passport size)
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- Watumishi wa umma wasiohitajika kuomba.
- Mwisho wa kupokea maombi: 17 Juni, 2025
- Waombaji wenye ulemavu watapewa kipaumbele.
Imetolewa na:
Lydia M. Churi
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Tume ya Utumishi wa Mahakama
Simu: 0734 219 821 / 0738 247 341
Barua pepe: [email protected]
 sw-1749010368-TANGAZO AJIRA MPYA_03_6_2025_FS
Makala Nyingine:
Tags: Jsc Ajira portal login, JSC Ajira portal registration, Nafasi Za Kazi, Tume ya Utumishi wa Mahakama