Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Tarehe: 22 Oktoba, 2024
Kumb. Na: JA.9/259/01/B/90
Kwa niaba ya Makumbusho ya Taifa ya Tanzania (NMT) National Museum of Tanzania (NMT) , Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa stahiki kujaza nafasi 16 za ajira kama ifuatavyo:
1. Makumbusho ya Taifa ya Tanzania (NMT)
Makumbusho ya Taifa ya Tanzania ni taasisi ya kisayansi, elimu na utamaduni iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Makumbusho ya Taifa Na.7 ya mwaka 1980. Jukumu lake ni kukusanya, kuhifadhi, na kuelimisha kuhusu urithi wa kitamaduni na asili wa Tanzania. Makumbusho yana matawi saba na maeneo mbalimbali ya kihistoria nchini.
2. Nafasi za Kazi na Majukumu
1. Msaidizi wa Makumbusho II (Museum Attendant II) – Nafasi 3
- Majukumu:
- Kudumisha usafi wa maonesho.
- Kusimamia wageni katika kumbi za maonesho.
- Kuwatembeza wageni.
- Kufuatilia usalama wa maonesho.
- Sifa: Cheti cha Sekondari (CSEE), Kiswahili na Kiingereza, na Cheti cha Ukarimu, Utunzaji wa Urithi, au Uongozaji Watalii.
- Mshahara: PGSS 2.
2. Mhifadhi II (Conservator II – Museum Conservation) – Nafasi 2
- Majukumu:
- Kusaidia kutambua uharibifu wa makusanyo.
- Kurekodi hali ya mazingira kwenye kumbi.
- Kushiriki kurekebisha makusanyo yaliyoathirika.
- Sifa: Shahada ya Baiolojia, Botania, Kemia, Usimamizi wa Urithi au Arkeolojia.
- Mshahara: PGSS 6.
3. Mhifadhi II (Conservator II – Monuments and Sites) – Nafasi 2
- Majukumu:
- Kukusanya data za utafiti na kuingiza kwenye kompyuta.
- Kuandaa ripoti za kiufundi na maombi ya miradi ya utafiti.
- Sifa: Shahada ya Kemia, Uhandisi wa Kemia, Jiolojia au Usimamizi wa Urithi.
- Mshahara: PGSS 6.
4. Mhifadhi II (Zoology) – Nafasi 1
- Majukumu:
- Kukusanya na kuhifadhi makusanyo ya wanyama.
- Kurekebisha maonesho na kuandaa mipango ya maonesho.
- Sifa: Shahada ya Zoolojia, Botania au Sayansi za Maji.
- Mshahara: PGSS 6.
5. Mhifadhi II (Historia) – Nafasi 2
- Majukumu:
Kama ya Mhifadhi II (Zoology). - Sifa: Shahada ya Historia.
- Mshahara: PGSS 6.
6. Msaidizi wa Utafiti II (Research Assistant II) – Nafasi 1
- Majukumu:
- Kukusanya na kuchambua data za utafiti chini ya usimamizi wa wataalamu wakuu.
- Kuandaa ripoti za utafiti na rasimu za maandiko.
- Sifa: Shahada ya Zoolojia.
- Mshahara: PRSS 1.
7. Afisa Utafiti II (Sanaa na Ubunifu) – Nafasi 1
- Majukumu:
Kufanya utafiti wa kisanaa na kuandaa maandiko. - Sifa: Shahada na Stashahada ya Uzamili katika Sanaa na Ubunifu.
- Mshahara: PRSS 2.
8. Afisa Utafiti II (Usanifu Majengo) – Nafasi 1
- Majukumu:
Kama ya Afisa Utafiti II (Sanaa na Ubunifu). - Sifa: Shahada na Stashahada ya Uzamili katika Usanifu Majengo.
- Mshahara: PRSS 2.
9. Fundi II (Plumbing) – Nafasi 2
- Majukumu:
- Kufanya matengenezo ya mifumo ya maji.
- Kufunga na kutengeneza miundombinu ya maji.
- Sifa: Cheti cha Trade Test katika Plumbing.
- Mshahara: PGSS 2.
Maelezo Zaidi Chukuwa PDF Hapa; NAFASI ZA KAZI MAKUMBUSHO YA TAIFA 23-10-2024
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Waombaji wawe raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45.
- Watu wenye ulemavu wanahimizwa kuomba.
- Maombi yaambatane na CV ya kisasa yenye mawasiliano ya uhakika.
- Vyeti vya elimu ya sekondari na ngazi ya juu lazima viwe vimethibitishwa.
- Maombi yatolewe kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa ajira wa serikali: http://portal.ajira.go.tz.
Mwisho wa kutuma maombi: 3 Novemba, 2024.
Imetolewa na: Katibu, Sekretarieti ya Ajira, Ofisi ya Rais
Nafasi Za Kazi Nyingine:
Leave a Reply