Nafasi za kazi JWTZ 2026 Kuandikishwa Jeshini

Nafasi za kazi JWTZ 2026/2027 Kuandikishwa na Kujiunga (Jeshi) Jeshini Nafasi za kazi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) 2026, NAFASI ZA KAZI JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) 2026

Kuandikishwa na Kujiunga Jeshini Mwaka 2026

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) halihusiki na wala halitoi ajira kwa njia ya rushwa au malipo ya fedha. Usikubali kumpa mtu yeyote pesa ili uombe au upewe ajira hizi. JWTZ linafuata taratibu rasmi na halali za kisheria katika kuwaandikisha vijana. Epuka matapeli.

TANGAZO LA AJIRA JWTZ 2026

Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Jacob John Mkunda, ametangaza nafasi za kuandikishwa jeshini kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu ya Sekondari hadi elimu ya Juu.

VIGEZO VYA MWOMBAJI

Jedwali lifuatalo linaonyesha vigezo vya elimu na umri kwa waombaji:

Kiwango cha Elimu Umri Usiozidi (Miaka)
Kidato cha Nne (Form IV) 24
Kidato cha Sita (Form VI) 24
Stashahada (Diploma) 26
Shahada ya Chuo Kikuu (Degree) 27
Madaktari Bingwa 35

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI

  • Maombi yaandikwe kwa mkono
  • Maombi yawasilishwe kwa mujibu wa utaratibu wa Jeshi, maeneo rasmi yatakayotajwa na JWTZ

VIAMBATANISHO VYA LAZIMA

Waombaji wote wanatakiwa kuambatisha nyaraka zifuatazo:

  1. Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) na namba ya NIDA
  2. Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa
  3. Vyeti vya elimu ya sekondari (Kidato cha Nne/Sita)
  4. Vyeti vya elimu ya juu (Stashahada/Shahada)
  5. Namba ya simu inayopatikana kwa urahisi

ANGALIZO KUTOKA JWTZ

“Nitoe angalizo kwa wananchi, hakuna nafasi ya kuandikishwa jeshini kwa kutoa fedha. Msikubali kutapeliwa.”
Kanali Gaudentius Ilonda

Kwa taarifa zaidi na utaratibu wa maombi, tembelea:
🔗 www.tpdf.mil.tz

Makala Nyingine: