Nafasi za kazi JWTZ 2025 Kuandikishwa na Kujiunga (Jeshi) Jeshini Nafasi za kazi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) 2025, NAFASI ZA KAZI JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) 2025
Kuandikishwa na Kujiunga Jeshini Mwaka 2025
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) halihusiki na wala halitoi ajira kwa njia ya rushwa au malipo ya fedha. Usikubali kumpa mtu yeyote pesa ili uombe au upewe ajira hizi. JWTZ linafuata taratibu rasmi na halali za kisheria katika kuwaandikisha vijana. Epuka matapeli.
TANGAZO LA AJIRA JWTZ 2025
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Jacob John Mkunda, ametangaza nafasi za kuandikishwa jeshini kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu ya Sekondari hadi elimu ya Juu. Tangazo hili limetolewa leo tarehe 30 Aprili 2025, makao makuu ya JWTZ yaliyopo Msalato, Dodoma, kupitia msemaji wa Jeshi, Kanali Gaudentius Ilonda.
VIGEZO VYA MWOMBAJI
Jedwali lifuatalo linaonyesha vigezo vya elimu na umri kwa waombaji:
Kiwango cha Elimu | Umri Usiozidi (Miaka) |
---|---|
Kidato cha Nne (Form IV) | 24 |
Kidato cha Sita (Form VI) | 24 |
Stashahada (Diploma) | 26 |
Shahada ya Chuo Kikuu (Degree) | 27 |
Madaktari Bingwa | 35 |
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
- Maombi yaandikwe kwa mkono
- Muda wa kuwasilisha maombi: 01 Mei 2025 hadi 14 Mei 2025
- Maombi yawasilishwe kwa mujibu wa utaratibu wa Jeshi, maeneo rasmi yatakayotajwa na JWTZ
VIAMBATANISHO VYA LAZIMA
Waombaji wote wanatakiwa kuambatisha nyaraka zifuatazo:
- Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) na namba ya NIDA
- Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa
- Vyeti vya elimu ya sekondari (Kidato cha Nne/Sita)
- Vyeti vya elimu ya juu (Stashahada/Shahada)
- Namba ya simu inayopatikana kwa urahisi
ANGALIZO KUTOKA JWTZ
“Nitoe angalizo kwa wananchi, hakuna nafasi ya kuandikishwa jeshini kwa kutoa fedha. Msikubali kutapeliwa.”
— Kanali Gaudentius Ilonda
Kwa taarifa zaidi na utaratibu wa maombi, tembelea:
🔗 www.tpdf.mil.tz
Makala Nyingine:
Leave a Reply