Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Mvomero 27-05-2025, Kumb. Na. MDVC/L.10/22/53 | Tarehe: 27 Mei, 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero anapokea maombi ya ajira kwa Watanzania wote wenye sifa, kufuatia kibali cha ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1.0 NAFASI ZINAZOTANGAZWA
1.1 Dereva Daraja la II – Nafasi 7
Majukumu ni pamoja na:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari;
- Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;
- Kuandika taarifa za safari kwenye log book;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kufanya usafi wa gari;
- Kufanya kazi nyingine kadri ya maelekezo kutoka kwa msimamizi.
Sifa za mwombaji:
- Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV);
- Leseni ya daraja “C” au “E”;
- Uzoefu wa angalau mwaka mmoja wa kuendesha gari bila ajali;
- Cheti cha mafunzo ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Ngazi ya mshahara: TGS B
1.2 Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 2
Majukumu ni pamoja na:
- Kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka kwenye masjala;
- Kusambaza na kupokea majalada kutoka kwa watendaji;
- Kurudisha na kuhifadhi majalada sehemu husika;
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi.
Sifa za mwombaji:
- Cheti cha Kidato cha Nne au Sita;
- Stashahada (NTA Level 6) ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali;
- Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
Ngazi ya mshahara: TGS C
2.0 MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45.
- Aambatishe maelezo binafsi ya kutosha (CV), anuani ya barua, namba za simu, barua pepe, na majina ya wadhamini watatu.
- Awasilishe nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili:
- Cheti cha kidato cha IV au VI,
- Cheti cha taaluma husika,
- Cheti cha kompyuta (ikihitajika),
- Vyeti vya kitaaluma.
- Hati kama “Testmonial”, “Provisional Results”, “Statement of Results”, au slips za matokeo hazitakubaliwa.
- Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na mamlaka husika (NECTA, NACTE, TCU).
- Waliostaafu hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji watakaowasilisha taarifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 03 Juni, 2025.
3.0 NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Barua ya maombi ya kazi iwe imeandikwa kwa ufasaha, imeambatanishwa na vyeti vyote muhimu, na ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero
S.L.P. 663, MOROGORO
Maombi yote yawasilishwe kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal):
👉 https://portal.ajira.go.tz
Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo huu hayatafanyiwa kazi.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero
Makala Nyingine: