Nafasi Za Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Novemba, 2024

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuomba nafasi ya kazi iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb Na. FA. 170/363/01A/116 cha tarehe 25 Septemba, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Ummana Utawala Bora.

MHUDUMU WA JIKONI DARAJA II- (NAFASI 4)

  • MAJUKUMU YA KAZI
    1. Kusafisha vyombo vya kupikia;
    2. Kusafisha vyombo vya kulia chakula;
  • Kusafisha sehemu ya kulia chakula;
  1. Kuwatayarishia Wapishi/Waandazi vifaa vya kazi;
  2. Kusafisha maeneo ya kupikia.

SIFA ZA KUAJIRIWA

Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV)

Mwenye cheti cha mafunzo ya mwaka mmoja ya Uhudumu wa Jikoni kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali

Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa S.L.P 162 Simu Na: 026 – 2702647, Barua Pepe:md@iringamc.go.tz, Tovuti: www.iringamc.go.tz

NGAZI YA MSHAHARA

Ngazi ya mshahara ni TGOS A

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini;
  2. Waombaji wenye ulemavu   wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili;
  1. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe
  2. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  3. Maombi yote yaambatane na cheti cha taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne na cheti cha kuhitimu mafunzo ya Uhudumu wa
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne (FORM IV AND RESULTS SLIPS)

viii.    Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).

  1. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  2. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  3. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
  • Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 02/12/2024.

Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa S.L.P 162 Simu Na: 026 – 2702647, Barua Pepe:md@iringamc.go.tz, Tovuti:www.iringamc.go.tz

  • Muhimu: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

Mkurugenzi wa Halmashauri, Manispaa ya Iringa,

S.L.P. 162, IRINGA.

  1. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal)

kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

vi.  Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Tangazo hili limetolewa na;

MKURUGENZI WA HALMASHAURI MANISPAA YA IRINGA.

Makala Nyingine: