Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Itigi 22-05-2025, HALMASHAURI YA WILAYA YA ITIGI inawatangazia Watanzania wote wenye sifa za kuajiriwa katika nafasi zifuatazo za kazi, kufuatia kibali kilichotolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1. Dereva Daraja la II – Nafasi 4
Sifa za Muombaji:
- Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV)
- Leseni ya Daraja E au C
- Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya ufundi stadi (VETA) au chuo kinachotambuliwa na serikali
- Awe ameendesha gari kwa mwaka mmoja au zaidi bila kusababisha ajali
Majukumu ya Kazi:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari
- Kuwapeleka watumishi katika safari za kikazi
- Kufanya matengenezo madogo ya gari
- Kusambaza nyaraka mbalimbali
- Kutunza daftari la safari
- Kufanya usafi wa gari
- Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa
Ngazi ya Mshahara: TGS B (kwa mujibu wa mishahara ya Serikali)
2. Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
- Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45
- Aambatishe cheti cha kuzaliwa
- Awasilishe wasifu binafsi (CV) yenye anuani, simu, na wadhamini
- Awe na nakala za vyeti vya taaluma husika na vya Kidato cha Nne na/au Sita
- HAKUBALIKI: Statement of Results au Provisional Results
- Aweke picha mbili za “passport size” kwenye mfumo
- Vyeti vya nje ya nchi vihakikiwe na TCU, NECTA au NACTE
- Waliofukuzwa kazi au kustafu bila kibali hawaruhusiwi kuomba
- Taarifa au vyeti vya kughushi ni kosa la jinai
3. Jinsi ya Kutuma Maombi:
Tuma maombi kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira:
https://portal.ajira.go.tz/
Maombi yaambatane na barua ya maombi iliyosainiwa, vyeti vya elimu, na vielelezo vyote muhimu.
Anuani ya barua iwe kama ifuatavyo:
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Itigi,
01 Barabara ya Halmashauri,
S.L.P 70,
43483 ITIGI – SINGIDA.
Tangazo hili limetolewa na:
Ayoub J. Kambi
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Makala Nyingine: