Msimamo wa Makundi CHAN 2025 Fixtures

Msimamo wa Makundi ya CHAN 2025 Fixtures, (Kundi la Taifa stars), Michuano ya CHAN 2025 inaendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali barani Afrika, ikiwa katika hatua ya makundi ambapo mataifa shiriki yanapambana vikali kuhakikisha yanapata nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali.

Mashindano haya yamevutia hisia za mashabiki kutokana na ushindani mkali na matokeo yasiyotabirika, huku kila timu ikionesha dhamira ya kulitafuta taji la mwaka huu.

Hali ya msimamo wa makundi inazidi kubadilika kadri michezo inavyoendelea, na tayari baadhi ya timu zimeanza kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu, huku nyingine zikikabiliwa na presha ya kupata matokeo chanya katika michezo iliyosalia.

Msimamo wa Makundi CHAN 2025

Kundi A

Nafasi Taifa Pointi
1 Kenya 7
2 Angola 4
3 DR Congo 3
4 Morocco 3
5 Zambia 0

Kundi B

Nafasi Taifa Pointi
1 Tanzania 9
2 Mauritania 4
3 Burkina Faso 3
4 Madagascar 1
5 Afrika ya Kati 0

Kundi C

Nafasi Taifa Pointi
1 Uganda 6
2 Algeria 4
3 Afrika Kusini 4
4 Guinea 3
5 Niger 0

Kundi D

Nafasi Taifa Pointi
1 Senegal 3
2 Congo 1
3 Sudan 1
4 Nigeria 0

Kwa sasa, Tanzania na Kenya ndizo zinazoongoza makundi yao bila shaka, zikiwa na nafasi kubwa ya kutinga robo fainali. Senegal nayo imeanza vyema Kundi D, huku Uganda ikiongoza Kundi C kwa ushindi muhimu.

Upande wa pili wa meza, timu kama Zambia na Niger ziko kwenye hali ngumu, zikihitaji miujiza ili kusalia kwenye michuano. Kadri michezo inavyoendelea, kila alama inakuwa muhimu na msisimko wa CHAN 2025 unaendelea kupanda.