Kusitishwa Kwa Usaili Kwa Kada Za Ualimu Oct 17, 2024

Kusitishwa Kwa Usaili Kwa Kada Za Ualimu Oct 17, 2024 (Usaili kwa Maana Nyingine interview ya Walimu imesitishwa.

Katibu – Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, anapenda kuwatangazia waombaji wote wa kazi za Kada za Ualimu ambao walikuwa wameitwa kwenye usaili kupitia tangazo la tarehe 15 Oktoba, 2024 kuwa usaili huo umesitishwa kwa sasa hadi watakapojulishwa tena.

Tangazo la awali lilionesha kuwa usaili wa Kada za Ualimu ulipangwa kuanza tarehe 23 Oktoba hadi 19 Novemba, 2024. Hata hivyo, kwa sasa usaili huo umesitishwa kwa sababu maalum, na taarifa zaidi zitatolewa kwa wakati muafaka.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya.

Lynn Chawala

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Simu: 255 (026) 2963652
Tovuti: www.ajira.go.tz
Barua Pepe: katibu@ajira.go.tz

Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma
Jengo la Utumishi (UDOM)
Eneo la Dkt. Asha Rose Migiro
S.L.P. 2320,
Dodoma

Imetolewa: Oktoba 17, 2024
Mahali: Dodoma

Makala Nyingine: