Haya Hapa Matokeo ya Kidato Cha Nne 2024/2025 Baraza la Mitihani (NECTA), Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika November 2024 ambapo jumla ya Watahiniwa wa Shule 477,262 kati ya 516,695 wenye matokeo ambao ni sawa na asilimia 92.37 wamefaulu ambapo.
wamepata madaraja ya I, II, III na IV.
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Said Mohamed
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dkt. Said Mohamed ametangaza matokeo hayo leo January 23,2025 Jijini Dar es salaam ambapo amesema mwaka 2023 Watahiniwa waliofaulu walikuwa 471,427 sawa na asilimia 89.36, hivyo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.01 na kwamba kati ya Watahiniwa 477,262 waliofaulu, Wasichana ni 249,078 sawa na asilimia 91.72 ya Wasichana wote wenye matokeo na Wavulana ni 228,184 sawa na asilimia 93.08 ya Wavulana wote wenye matokeo.
Matokeo Na Link inayofunguka ya MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024
Hapa chini:Â
Matokeo Kidato Cha Nne 2024/2025 (CSEE Form Four Results)
NECTA Yatangaza Matokeo ya kidato cha nne 2024/2025 (Form Four Results CSEE)
Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato cha nne 2024 (form Four)
Matokeo ya Kidato Cha Nne 2024/2025 (Form Four Results)
Link inayofunguka ya Matokeo ya Kidato cha nne 2024
https://matokeo.necta.go.tz/results/2024/csee/CSEE2024/CSEE2024.htm
Kwa upande wa Watahiniwa wa Kujitegemea waliofaulu mtihani ni 15,703 sawa na asilimia 62.51 ambapo mwaka 2023 Watahiniwa wa Kujitegemea 13,396 sawa na asilimia 52.44 walifaulu mtihani huo, hivyo ufaulu wa Watahiniwa wa Kujitegemea umepanda kwa asilimia 10.07 ikilinganishwa na mwaka 2023.
Leave a Reply