Fani Na Kada Za zinazohitajika Ajira Za JWTZ 2025

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za kuandikishwa jeshini kwa vijana wa Kitanzania waliomaliza elimu ya sekondari hadi elimu ya juu, hususan wale wenye ujuzi maalum na taaluma za kitabibu na kiufundi.

Tangazo hili limetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano, Kanali Gaudentius Ilonda, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi, Msalato jijini Dodoma.

Fani Zinazohitajika JWTZ 2025

Jedwali lifuatalo linaonyesha kada na fani mbalimbali za kitaalamu zinazohitajika kwa ajili ya kuandikishwa jeshini:

Namba Fani / Kada Inayohitajika
1 Daktari wa Upasuaji Mkuu
2 Daktari wa Upasuaji wa Mifupa na Viungo
3 Daktari wa Magonjwa ya Kibofu na Njia ya Mkojo
4 Mtaalamu wa Picha za Magonjwa (X-ray, MRI, CT)
5 Daktari wa Masikio, Pua na Koo (ENT)
6 Daktari wa Usingizi
7 Daktari wa Magonjwa ya Ndani
8 Daktari wa Macho
9 Daktari wa Saratani
10 Daktari wa Uchunguzi wa Sampuli za Mwili
11 Daktari wa Magonjwa ya Akili
12 Daktari wa Huduma za Dharura
13 Daktari wa Magonjwa ya Damu
14 Daktari wa Tiba za Wanyama
15 Mhandisi wa Tiba na Vifaa-Tiba
16 Mtaalamu wa Maabara ya Meno
17 Daktari wa Afya za Abiria na Wahudumu wa Anga
18 Fundi Mchundo – Aluminium Welding
19 Fundi wa Welding na Metal Fabrication

Sifa Za Waombaji

Waombaji wote wanapaswa kuwa na sifa zifuatazo:

  • Awe Mtanzania halali mwenye Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
  • Awe na afya njema na akili timamu
  • Asiwe amehukumiwa kwa kosa lolote la jinai
  • Awe na cheti halisi cha kuzaliwa
  • Awe na vyeti vya kitaaluma na vya shule
  • Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo, au Kikosi cha Kuzuia Magendo
  • Awe amehitimu JKT (kwa mujibu wa sheria) na ana cheti cha kuthibitisha

Umri Unaokubalika Kulingana na Elimu

Kiwango cha Elimu Umri Usiozidi (Miaka)
Kidato cha Nne (Form IV) 24
Kidato cha Sita (Form VI) 24
Stashahada (Diploma) 26
Shahada ya Chuo Kikuu (Degree) 27
Madaktari Bingwa 35

Utaratibu wa Kutuma Maombi

  • Maombi yaandikwe kwa mkono
  • Yawasilishwe kuanzia Mei 1 hadi Mei 14, 2025
  • Yapelekwe Makao Makuu ya JWTZ, Msalato – Dodoma

Viambatisho vya Lazima kwa Maombi

  1. Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba yake
  2. Nakala ya cheti cha kuzaliwa
  3. Vyeti vya shule na taaluma
  4. Cheti cha JKT kwa waliomaliza mkataba wa kujitolea
  5. Namba ya simu ya mkononi ya mwombaji kwa ajili ya mawasiliano

Kwa taarifa zaidi tembelea:
🔗 www.tpdf.mil.tz

Makala Nyingine:

Nafasi za kazi JWTZ 2025 Kuandikishwa Jeshini

Sifa za kujiunga na JWTZ (Jeshi La Wananchi Wa Tanzania)

JWTZ Vyeo na Mishahara

Jinsi ya Kujiunga na JKT (Mwongozo kamili)