Makala Ya Leo Kuhusu Matokeo Na Kikosi; Simba vs Yanga SC Leo – 16 Septemba 2025 (Matokeo ya Simba na Yanga Live Results Today) Ngao Ya Jamii Kuashiria Kuanza Kwa Mzunguko Wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara. Simba vs yanga 16 september 2025
Septemba 16, 2025, dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam limefurika mashabiki wa soka kushuhudia fainali ya Ngao ya Jamii 2025. Hii ni mechi ya kufungua rasmi msimu mpya wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2025/2026, ikiwakutanisha mahasimu wakubwa wa soka la Tanzania, Simba SC na Yanga SC.
Mchezo huu unatabiriwa kuwa na msisimko mkubwa kutokana na historia, rekodi na ushindani mkali wa timu hizi mbili kongwe.
Ngao ya Jamii 2025
Ngao ya Jamii imekuwa sehemu muhimu ya ratiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tangu ilipoanzishwa mwaka 2001.
- Awali, ilikuwa ni kati ya bingwa wa ligi na mshindi wa Kombe la FA.
- Miaka ya karibuni ilihusisha timu nne, lakini kwa msimu huu TFF imepunguza idadi ya washiriki kutokana na ratiba ngumu za kimataifa na kitaifa.
Kwa mwaka huu, shindano hili limewaleta pamoja Simba na Yanga pekee, ili kupunguza msongamano wa michezo, hasa kutokana na majukumu ya klabu kwenye mashindano ya CAF na pia ratiba ya Taifa Stars kuelekea mchujo wa Kombe la Dunia 2026.
Rekodi za Simba na Yanga Katika Ngao ya Jamii
- Simba SC
- Imechukua Ngao ya Jamii mara 10.
- Ushindi wa kwanza ulikuwa mwaka 2002 dhidi ya Yanga (4-1).
- Ushindi wa karibuni: 2023, waliibuka kidedea kwa penalti 3-1 baada ya sare tasa.
- Yanga SC
- Imeshinda Ngao ya Jamii mara 8.
- Ushindi wa kwanza ulikuwa mwaka 2001 dhidi ya Simba (2-1).
- Ushindi wa karibuni: 2024 dhidi ya Azam FC (4-1).
Kwa ujumla, timu hizi zimekutana mara 9 kwenye fainali za Ngao ya Jamii:
- Simba imeshinda mara 5.
- Yanga imeshinda mara 4.
Hii inafanya fainali ya 2025 kuwa na mvuto wa pekee: Simba inalenga kuongeza uongozi, huku Yanga ikiwinda kusawazisha rekodi.
Kikosi Cha Simba SC Leo – 16 Septemba 2025
- Moussa Camara
- Ladack Chasambi
- Antony Mligo
- Rushine De Reuck
- Karaboue Chamou
- Abdurazack Hamza
- Kibu Denis (C)
- Naby Camara
- Jonathan Sowah
- Jean Charles Ahoua
- Neo Maema
Mechi ya Derby ya Kariakoo
- Tarehe: 16 Septemba 2025
- Uwanja: Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
- Muda: Saa 11:00 jioni (EAT)
- Shindano: Ngao ya Jamii 2025
DERBY DAY – #KariakooDerby
Mashabiki kote nchini na kanda ya Afrika Mashariki wanatarajia pambano la kiwango cha juu kati ya miamba hii miwili ya soka.
Matokeo ya Moja kwa Moja (Live Results)
👉 Bofya Hapa Kutazama Live Matokeo
Makala Nyingine:
Tuachie Maoni Yako