Kuitwa Kwenye Usaili Halmashauri Ya Manispaa Ya Temeke Juni, 2025

Filed in Ajira by on June 15, 2025 0 Comments

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE 13-06-2025, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke anawatangazia waombaji wa nafasi ya Dereva Daraja la II kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 24 hadi 27 Juni 2025. Waombaji walioitwa wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI – HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE
Tarehe: 13 Juni 2025
Kumb. Na: TMC/MD/B.2/37/89

Maelekezo kwa Wasailiwa:

  1. Fika kwa wakati, siku na mahali kama ilivyoelekezwa kwenye ratiba ya usaili.

  2. Kuvaa barakoa (mask) ni lazima.

  3. Kuja na kitambulisho halali (Uraia, Kazi, Mpiga Kura, Pasipoti).

  4. Leta vyeti halisi: Cheti cha kuzaliwa, Kidato cha IV, Astashahada na Leseni ya Udereva.

  5. Hati zifuatazo hazitakubalika: Testimonials, Provisional Results, Statement of Results, na slips za matokeo.

  6. Gharama za chakula, usafiri na malazi ni kwa msailiwa mwenyewe.

  7. Vyeti kutoka nje ya Tanzania viwe vimehakikiwa na TCU, NACTE au NECTA.

  8. Wasailiwa wasioonekana kwenye tangazo hili hawakukidhi vigezo.

  9. Dereva Daraja II wenye leseni Daraja C au E lazima waje na vyeti vya mafunzo ya udereva.

  10. Ikiwa jina linatofautiana kwenye vyeti, leta Hati ya kiapo ya kubadilisha jina (Deed Poll).

  11. Ingia kwenye akaunti yako ya ajira ili kunakili namba ya mtihani – haitatolewa siku ya usaili.

Ratiba ya Usaili – Dereva Daraja la II:

Aina ya Usaili Tarehe Saa Mahali
Usaili wa Mchujo 24-06-2025 07:00 Asubuhi Ukumbi wa Idd Nyundo – Manispaa ya Temeke
Usaili wa Vitendo 26-06-2025 07:00 Asubuhi Ukumbi wa Idd Nyundo – Manispaa ya Temeke
Usaili wa Mahojiano 27-06-2025 07:00 Asubuhi Ukumbi wa Idd Nyundo – Manispaa ya Temeke

Majina ya Wasailiwa (Mifano):

Orodha ina zaidi ya waombaji 190, baadhi yao ni:

  • ABDALAH HUSENI ADIMU – P.O Box 14, Songea, Ruvuma

  • ABDUBAKAR BIZIMANA TOMSON – P.O Box 40, Mvomero, Morogoro

  • ABIHUDY EZEKIEL KANYANYI – P.O Box 6013, Morogoro

  • ADAM ZUBERI KAMBI – P.O Box 20950, Ubungo, Dar es Salaam

  • CAROLINE PETER MARTINE – P.O Box 2052, Ubungo, Dar es Salaam

  • JOYCE REMENI MUSHI – P.O Box 166, Morogoro

  • ZABLON SANNE MICHAEL – P.O Box 12702, Dodoma

…na wengine wengi waliotajwa kwenye tangazo kamili.

Imetolewa na:
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke
Ofisi ya Rais – TAMISEMI

TANGAZO LA USAILI TEMEKE MC.pdf

Makala Nyingine:

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.