Tangazo hili limetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano, Kanali Gaudentius Ilonda, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi, Msalato jijini Dodoma.
Fani Zinazohitajika JWTZ 2025
Jedwali lifuatalo linaonyesha kada na fani mbalimbali za kitaalamu zinazohitajika kwa ajili ya kuandikishwa jeshini:
Namba | Fani / Kada Inayohitajika |
---|---|
1 | Daktari wa Upasuaji Mkuu |
2 | Daktari wa Upasuaji wa Mifupa na Viungo |
3 | Daktari wa Magonjwa ya Kibofu na Njia ya Mkojo |
4 | Mtaalamu wa Picha za Magonjwa (X-ray, MRI, CT) |
5 | Daktari wa Masikio, Pua na Koo (ENT) |
6 | Daktari wa Usingizi |
7 | Daktari wa Magonjwa ya Ndani |
8 | Daktari wa Macho |
9 | Daktari wa Saratani |
10 | Daktari wa Uchunguzi wa Sampuli za Mwili |
11 | Daktari wa Magonjwa ya Akili |
12 | Daktari wa Huduma za Dharura |
13 | Daktari wa Magonjwa ya Damu |
14 | Daktari wa Tiba za Wanyama |
15 | Mhandisi wa Tiba na Vifaa-Tiba |
16 | Mtaalamu wa Maabara ya Meno |
17 | Daktari wa Afya za Abiria na Wahudumu wa Anga |
18 | Fundi Mchundo – Aluminium Welding |
19 | Fundi wa Welding na Metal Fabrication |
Sifa Za Waombaji
Waombaji wote wanapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
- Awe Mtanzania halali mwenye Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- Awe na afya njema na akili timamu
- Asiwe amehukumiwa kwa kosa lolote la jinai
- Awe na cheti halisi cha kuzaliwa
- Awe na vyeti vya kitaaluma na vya shule
- Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo, au Kikosi cha Kuzuia Magendo
- Awe amehitimu JKT (kwa mujibu wa sheria) na ana cheti cha kuthibitisha
Umri Unaokubalika Kulingana na Elimu
Kiwango cha Elimu | Umri Usiozidi (Miaka) |
---|---|
Kidato cha Nne (Form IV) | 24 |
Kidato cha Sita (Form VI) | 24 |
Stashahada (Diploma) | 26 |
Shahada ya Chuo Kikuu (Degree) | 27 |
Madaktari Bingwa | 35 |
Utaratibu wa Kutuma Maombi
- Maombi yaandikwe kwa mkono
- Yawasilishwe kuanzia Mei 1 hadi Mei 14, 2025
- Yapelekwe Makao Makuu ya JWTZ, Msalato – Dodoma
Viambatisho vya Lazima kwa Maombi
- Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba yake
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa
- Vyeti vya shule na taaluma
- Cheti cha JKT kwa waliomaliza mkataba wa kujitolea
- Namba ya simu ya mkononi ya mwombaji kwa ajili ya mawasiliano
Kwa taarifa zaidi tembelea:
🔗 www.tpdf.mil.tz
Makala Nyingine:
Nafasi za kazi JWTZ 2025 Kuandikishwa Jeshini
Leave a Reply