Majina ya walioitwa kazini Afya 2025 TAMISEMI

Majina ya walioitwa kazini Afya 2025 TAMISEMI 2025/2026 (TMCHIP), TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA AFYA – TAMISEMI 2025 PDF orodha ya Majina (list Nzima) (Tanzania Maternal and Child Health Investment Program (TMCHIP) Waliopata ajira kada ya Afya.

Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) inapenda kuwataarifu waombaji wote wa kazi za mkataba katika programu ya Mpango wa Uwekezaji katika Afya ya Mama na Mtoto nchini Tanzania (Tanzania Maternal and Child Health Investment Program (TMCHIP) waliowasilisha maombi ya ajira kwa nafasi mbalimbali za kada za afya katika kipindi cha mwezi wa Desemba, 2024 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilika hivyo waombaji wote waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti katika Halmashauri walizopangiwa.

Majina Waliochaguliwa-waliopata ajira kada za afya

Waombaji wote walio pata nafasi wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

Kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili. Aidha, waombaji watakaoshindwa kuripoti kwenye vituo vya kazi ndani ya siku kumi na nne (14) nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine haraka iwezekanavyo;

Kuwasilisha Vyeti Halisi (Original Certificates) vya Kidato cha Nne, Sita, Chuo Kikuu, NACTE na vyeti halisi vya usajili wa mabaraza ya kitaaluma kwa ajili ya kuhakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira;

Waombaji waliopata nafasi za ajira watakaoripoti bila ya kuwa na Vyeti Halisi (Original Certificates) vya Kidato cha Nne, Kidato Sita, Chuo Kikuu, NACTE na vyeti halisi vya usajili wa mabaraza ya kitaaluma hawatapokelewa;

Waombaji waliopata nafasi za ajira wanajulishwa kuwa hakutakuwa na nafasi ya kubadilisha vituo vya kazi walivyopangiwa.

Waombaji wote ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili, watambue kuwa hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaelekezwa kuwapokea, kuhakiki vyeti na kuwafanyia mafunzo elekezi (Induction Course) kabla ya kuwapangia vituo vya kazi.

Orodha ya majina ya waombaji waliopangiwa vituo vya kazi inapatikana kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI www.tamisemi.go.tz

Limetolewa na:

Katibu Mkuu,

Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mji wa Serikali – Mtumba,

S.L.P. 1923,

DODOMA.

15 Machi, 2025

PDF Ya Majina Ya Afya waliochagulliwa TAMISEMI

PDF TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA TMCHIP 2025

Mapendekezo:

  1. Walimu Walioitwa Kazini 2025/2026 Kupitia Ajira Portal
  2. Majina Ya Walioitwa Kazini Utumishi Na Ajira Portal 2025
  3. Majina Ya Waliopata Ajira Kada Ya Afya Oktoba 18, 2024
  4. Ajira Mpya za Walimu 2025/2026 Ajira Portal kutoka MDAs ; LGAs