Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Ileje 20-02-2025 Ajira mpya kutoka wilaya ya ILEJE zote pia unaweza kuzipata kwenye mfumo wa PDF.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kuomba nafasi ya kazi zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 10
- MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari; na
- Kufanya Usafi wa
1.1.1 SIFA ZA MWOMBAJI
Awe mwenye Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.2 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali – TGS B
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- “Testmonials”,” Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji walisoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za
- Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 06 Machi, 2025
- MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Ileje,
S.L.P 2, ILEJE.
- Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/(Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”).
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Tangazo hili limetolewa na;
Mkurugenzi Mtendaji (W) ILEJE
Chukua PDF Hapa; TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA ILEJE 20-02-2025
Nafasi Za kazi Nyingine:
- Nafasi Za Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Novemba, 2024
- Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Manispaa Ya Bukoba 22-10-2024
- Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Hanang 23-10-2024
- Tangazo La Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Kyela 21-10-2024
- Majina Ya Walioitwa Kazini Utumishi Na Ajira Portal 2025
Leave a Reply