Majina ya Walimu Walioitwa Kazini 2025/2026 Kupitia Ajira Portal (orodha na list ya majina kwenye PDF walioajiriwa 2025 na vituo vyao vya kazi) Majina ya walimu waliopata kazi 2025 MAJINAYA WALIOITWA KAZINI WALIMU KADA ZA UALIMU.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 14-08-2024 na tarehe 17-01-2025 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili.
Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Majina ya Walimu Walioitwa Kazini 2025
Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.
Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite
kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.
MUHIMU:
Wanaokuja kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi wanapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:-
- Kitambulisho cha Uraia,
- Hati ya kusafiria,
- Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi,
- Kitambulisho cha Mpiga kura au
- Leseni ya Udereva.
Orodha Ya Majina Kamili:
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 02-04-2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 27-03-2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 25-03-2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 22-03-2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU 20-03-2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU 18-03-2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU 17-03-2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 14-03-2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 13-03-2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 12-03-2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 10-03-2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 06-03-2025
- TANGAZO LA KUITWA KAZINI WALIMU NA KADA MBALIMBALI 04-03-2025
Kwa taarifa zaidi tembelea; https://www.ajira.go.tz/
Makala Nyingine:
- Majina Ya Walioitwa Kazini Utumishi Na Ajira Portal 2025
- Majina Ya Waliopata Ajira Kada Ya Afya Oktoba 18, 2024
- Matokeo Ya Usaili Wa Kuandika Mwalimu Daraja La Iii b (kemia, Baiolojia,tehama, Jiografia) Na Mwalimu Daraja La Iiia Elimu Ya Awali
- Matokeo Ya Usaili Wa Kuandika Mwalimu Daraja La III C Kiswahili
- Ratiba Ya Usaili wa Walimu 2025 (Kada Za Ualimu)
- Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI Na Ajira Portal 2025
- Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato cha nne 2024 (form Four)
- Matokeo ya Usaili Ajira Portal 2025, Matokeo ya Utumishi wa Umma, Serikalini
Mimi jamani mbona sijapangwa na nilihitimi chuo 2016??Nisaidieni na Mimi mtoto wa mkulima hata mlo mmija ni shida.
Serikali yangu nchi yangu naipenda Sana tangu nimehitimu chuo 2018 najitolea kufundisha shule ya serikali natekeleza majukumu yote kama ninavyopangiwa licha ya kila nikiomba kazi naachwa hakuna siku siend kazini na nina uhakika najituma mshahara hmna na sichoki najua ndicho mungu kanijalia na taarifa zangu mnazichukua tukumbukeni tunaojitolea maana hamjui tunayoyapitia
ulisoma masomo yapi?
Mbona ualimu daraja la IIIA, hayaonekani?
Yanatoka kidogokidogo
Mbona walio fanya usahili mtwara sija muona hata mmoja?
Idadi mbona ni ndogo sana? Au zinatoka kwa awamu?
Pia, walimu waliokuwemo kwenye database ni wenye sifa zipi? Wamefaulu written na oral interview au ni wa miaka ya nyumba?
Serikali tunaomba na sisi watu wa pharmacy mtusaidie tumekaa sana mtaani ht mitaji hatuna na tunategemewa mtukumbuke na sisi halo ni mbaya sana
Mbona walio fanya usahili mtwara sijamuona hata mmoja?
Kwani kujua umefaulu oral inakuaje maana me sijui jaman
Serikali tunaomba na sisi watu wa pharmacy hasa sisi pharm tech mtaani kugumu sana na familia zinatutegemea na mitaji ni changamoto mtupe nasi ajira tunaomba.
Aisee mbna mnatoa majina kidogokidogo sana ,toeni majina mengi ili mtu ajue kuwa apepangwa au hajapangwa afanye mambo mengine .
Aisee mbna mnatoa majina kidogokidogo sana ,toeni majina mengi ili mtu ajue kuwa apepangwa au hajapangwa afanye mambo mengine .
Naomba na mm basi ata jina langu liandikwe uko maan daah naumia kuona Majin ya wengine TU
Maisha ni magumu mtaani serikal tunaomba mtuangalie kwa jicho la pili miaka nane mtaani had vyeti vinazeeka duuh
Jmn serikal naomb waendelee kutoa majna ya Elimu ya Awali maan cna amani kabis familia inanitegemea na cna cha kufany naomb sana😭
Tunaomba muahiri walimu tuliofanyia njombe interview jaman
Jamani naombeni na mm Mungu awatangulie mtume na jina langu kwani mtaani ni pagimu jamani narudia kuangali mara tatutatu Wala jina silioni jamani tusaidieni
Kigoma mbona hawatoi jmn
EMANUEL PAULO. Tuna Imani na serikali yetu 💚 itatuajiri tu sisi walimu
walimu wa elimu ya awali mashulen hamna hadi wanachukuliwa walimu kazin waende semina kujifunza kufundisha elimu ya awali wakati sisi mmetuzalisha wengi lakin mnatuaacha mtaani mnachukua 20 tunaomba mtufikirie jamn🙏
Gloria Ferdinand
Serikali naomba mtuangalie tulio bahatika kuingia kwenye database maana bado tunasubiri hatima yetu
Samahan jaman naomba bas mtuajiri walimu tunaojitolea .. mfano mm nimejitolea huu ni mwaka wa tano nipo bado najitolea
Tunaomba muahiri walimu tuliofanyia njombe interview jaman
Tunaombeni mtuone na sisi
Tunaomba mzingatie wale waliofanyia interview mkoa Wa Kagera bukoba , maana naona hawazingatiwi