Walioitwa kwenye Usaili wa Mchujo TRA 2025 Majina Yametangazwa

Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili wa Mchujo pdf, Majina ya Walioitwa kwenye Usaili wa Mchujo TRA 2025, Call For interview TRA 2025. TRA SELECTED NAMES FOR WRITTEN INTERVIEW. 

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na.11 ya mwaka 1995 na kuanza rasmi tarehe 1 Julai 1996. Mamlaka hii imepewa jukumu la kutathmini, kukusanya, na kuhasibu mapato ya Serikali kwa mujibu wa sheria.

Kwa sasa, TRA inatekeleza Mpango Kazi wa Sita (CP6: 2022/23 – 2026/27) wenye Dira ya kuwa “Taasisi ya Mapato Inayoaminika kwa Maendeleo ya Jamii na Kiuchumi” na Dhamira ya “Kurahisisha na Kuimarisha Ulipaji Kodi wa Hiari kwa Maendeleo Endelevu”.

TARATIBU ZA USAILI

TRA inapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kati ya 06 Februari, 2025 – 19 Februari, 2025 kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 29 Machi, 2025.

Wasailiwa wote wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:

1. Tarehe na Mahali pa Usaili

Usaili utafanyika kwa mujibu wa tarehe, muda, na sehemu zilizoainishwa kwenye tangazo rasmi la TRA.

2. Barua ya Kuitwa Usaili

Kila msailiwa anatakiwa kuja na barua rasmi ya mwaliko yenye namba ya mtahiniwa iliyotumwa kwenye anuani yake ya barua pepe.

3. Kitambulisho Halali

Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa utambuzi:

  • ✔ Kitambulisho cha Uraia
  • ✔ Kitambulisho cha Mkaazi
  • ✔ Kitambulisho cha Mpiga Kura
  • ✔ Leseni ya Udereva
  • ✔ Hati ya Kusafiria
  • ✔ Barua ya Utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji

Vitambulisho tofauti na vilivyoainishwa havitatambuliwa!

4. Vyeti Halisi vya Elimu

Msailiwa anapaswa kufika na vyeti vyake halisi (Original Certificates) pamoja na nakala zake:

  • Cheti cha Kuzaliwa
  • Cheti cha Kidato cha IV na VI
  • Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea
  • Hati za matokeo za vyuo (Transcript)

📌 Wanaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of Results au Form V & VI Results Slips hawataruhusiwa kuendelea na usaili!

5. Vyeti kwa Waliosoma Nje ya Tanzania

  • Vyeti vyao vihalalishwe na mamlaka husika (TCU, NACTE au NECTA).

6. Usajili kwa Kada Maalum

  • Wale wanaotakiwa kuwa na usajili wa bodi za kitaaluma waje na vyeti vyao halisi vya usajili na leseni za kazi.

7. Uhakiki wa Vyeti

  • Uhakiki utaanza saa 12:00 asubuhi kwa ratiba ya asubuhi na saa 6:00 mchana kwa ratiba ya mchana.
  • Msailiwa ataruhusiwa kuendelea na usaili baada ya kuthibitisha vyeti na kuthibitishwa kuwa anastahili.

8. Gharama za Usaili

  • TRA haitatoa malipo yoyote kwa chakula, usafiri au malazi ya wasailiwa.

9. Mambo Yanayokatazwa

 Msailiwa haruhusiwi kuleta simu, saa au kifaa chochote cha kielektroniki kwenye eneo la usaili.

10. Wasailiwa Wenye Mahitaji Maalum

✔ Wanashauriwa kufika mapema na kuripoti kwa msimamizi wa kituo ili kupata msaada unaohitajika.

MUHIMU KWA WAOMBWAJI AMBAO MAJINA HAYAKUTOKEA KWENYE TANGAZO

📌 Kama jina lako halipo kwenye tangazo, inamaanisha hukukidhi vigezo vya awali.
Usikate tamaa! Unaweza kuomba tena nafasi mpya za kazi zitakapotangazwa.

PDF Ya Majina Hapo Chini

Orodha_ya_Walioitwa_kwenye_Usaili_wa_Mchujo.pdf

TRA logo

SELECTED NAMES FOR WRITTEN INTERVIEW

MAWASILIANO KWA TAARIFA ZAIDI

Tovuti: www.tra.go.tz
 Namba za simu bila malipo: 0800 780078 au 0800 750075
WhatsApp: 0744 23 33 33
Barua pepe: huduma@tra.go.tz au services@tra.go.tz

“Pamoja Tunajenga Taifa Letu!”

 Imetolewa na:
 Idara ya Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala – TRA

Makala Nyingine:

  1. Majina ya walioitwa kwenye usaili TRA 2025 (Call For interview)
  2. Maswali ya Usaili TRA Interview Questions 2025 PDF
  3. Mfumo Wa Ajira TRA (recruitment.tra.go.tz) recruitment Portal 2025
  4. Nafasi Za Kazi TRA 2025 Ajira Mpya 1592 Zilizotangazwa