Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Uhamiaji 2025

kwenye makala hii tutapata list (orodha kamili) ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Uhamiaji 2025 Waliochaguliwa  Usaili 2025/2026 wote. pia unaweza pata kwenye mfumo wa PDF.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia vijana walioomba Ajira kupitia Mfumo wa e-Ajira wa Uhamiaji na waliopokea barua pepe na ujumbe wa simu kufika kwenye usaili kama ifuatavyo:-

Waombaji walioombea Tanzania Bara wanatakiwa kufika katika Ukumbi wa Maktaba (Library) Ndaki ya Elimu (CoED) Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) tarehe 15 Januari, 2025 saa 1:00 asubuhi. Aidha, waombaji wa Zanzibar wanatakiwa kufika katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Hall uliopo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 15 Januari, 2025 saa 1:00 asubuhi.

Waombaji wote wanatakiwa kuwa na namba ya ombi la Ajira (Application ID) iliyochapishwa kama ilivyotumwa kwenye namba za simu na barua pepe, Kitambulisho chenye picha yake (Mfano, Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho cha Mkazi, Kadi ya Mpiga Kura, Pasipoti au Kitambulisho chochote kinachomtambulisha kwa sasa) pamoja na Kalamu ya wino wa bluu.

Kwa waombaji wenye fani za TEHAMA na ufundi magari wajiandae kwa usaili wa vitendo (Practical Examination).

Waombaji walioitwa kwenye usaili wamejulishwa kupitia namba zao za Simu na ujumbe wa barua pepe (e-mail) kama ilivyoainishwa katika Mfumo. Aidha, Wasailiwa wote watatakiwa kujigharamia chakula, usafiri na malazi wakati wote wa zoezi la usaili.

Aidha, Orodha ya Majina ya waliochaguliwa inapatikana kupitia tovuti ya Idara ya Uhamiaji (www.immigration.go.tz).

Limetolewa na;

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji 09 Januari, 2025

PDF Kamili Hapa: KUITWA-USAILI-UHAMIAJI-JANUARY-2025-

Makala Nyingine:

Nafasi za Kazi Uhamiaji 2024 Ajira Mpya