Walioitwa kwenye usaili TFS 2025

Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili 2025/2026 TFS kwenye PDF unaweza Ku-download, Waliochaguliwa TFS  Kamanda wa Kanda-Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) anapenda kuwataarifu waombaji wote walioomba kazi za Mkataba wa mwaka Mmoja kwa Tangazo lenye Kumb.AC.18/88/01B/42 la tarehe 12/08/2025

Usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 22/09/2025 Mpaka tarehe 23/09/2025 na hatimae kuwapatia ajira za Mkataba wa Mwaka Mmoja waombaji kazi watakaokuwa wamefaulu usaili huo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa.

Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili 2025/2026 TFS

Kuzingatia maelekezo yafuatayo;

1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe 22/09/2025 mpaka tarehe 23/09/2025 kama ilivyoonyeshwa kwenye Tangazo hili. Muda wa kuripoti kwa ajili ya usaili ni saa moja kamili asubuhi (01.00 Asubuhi). Sehemu ambapo usaili huu utafanyika, umeainishwa kwa kila Kada.

2. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi, kimojawapo kati ya Kitambulisho cha Uraia, Mpiga Kura, Leseni ya Udereva, hati ya Kusafiria au barua ya Serikali ya Mtaa.

3. Wasailiwa wanatakiwa kufika na vyeti vyao halisi vya kuzaliwa, Kidato cha IV, VI, Stashahada na Astashahada kulingana na sifa za Mwombaji.

4. Testimonials, Provisional results, statement of Results, Result slip hazitakubaliwa na HAWATORUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

5. Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi. Kila msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanya usaili.

7. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika Tangazo hili, watambue kuwa hawakukidhi vigezo, hivyo wasisite kuomba tena nafasi za kazi zitakapo tangazwa na kuzingatia mahitaji ya Tangazo.

PDF Walioitwa Kwenye Usaili TFS

KUITWA-KWENYE-USAILI-TFS-SEP-2025-elimuforum.com