Majina Ya Walioitwa kwenye Usaili Benki Kuu 2025 Tanzania BOT

Orodha ya Majina Ya Walioitwa kwenye Usaili Benki Kuu  BOT PDF 2025, TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI BENKI KUU YA TANZANIA 06-02-2025.

Naibu Gavana Utawala na Udhibiti wa Ndani wa Benki Kuu ya Tanzania anapenda kuwataarifu waombaji
kazi wote walioomba kazi kuwa usaili wa kuandika/mchujo (Aptitude Test) unatarajiwa kuendeshwa kuanzia
tarehe 15-02-2025 hadi 24-03-2025.

Walioitwa kwenye Usaili Benki Kuu 

Wasailiwa watakaofuzu usaili huu na kwenda katika hatua zinazofuata watatakiwa kushiriki katika usaili wa vitendo au/na mahojiano kwa tarehe iliyoanishwa au kama watakavyotaarifiwa kwa wakati husika.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wa kuandika/mchujo (Aptitude Test) wanapaswa kuzingatia maelekezo
yafuatayo:-

1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo
usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
3. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,
Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya
utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji/shehia anakotoka msailiwa.
4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI,
Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na vyeti vingine (kutegemeana na nafasi
aliyoomba).
5. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za
matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
6. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
7. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
8. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
Mamlaka husika (kama TCU, NACTVET au NECTA)
9. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya
tangazo husika.
10. Wasailiwa wa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja
na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
11. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba
ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
12. MUHIMU: Wasailiwa watakao shindwa kuwasilisha nyaraka zilizokamilika kama zilivyoainishwa katika
kipengele na. 2, 3, 4, 8 na 10 hawataruhusiwa kuendelea na usaili.

Majina PDF Walioitwa Kwenye Usaili Benki Kuu 2025

Makala Nyingine:

  1. Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI Na Ajira Portal 2025
  2. Matokeo ya Usaili Ajira Portal 2025, Matokeo ya Utumishi wa Umma, Serikalini
  3. Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Uhamiaji 2025
  4. Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili Wa Ajira Kwa Njia Ya Uhamisho NECTA