Ajira

Majina Ya Waliochaguliwa Kujiunga Na Jeshi La Polisi Tanzania 2025

Waliochaguliwa Kujiunga Na Jeshi La Polisi Tanzania 2025, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania anawatangazia vijana wote waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi kuwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kwa ajili ya kuanza mafunzo ya awali kwa tarehe na utaratibu ufuatao:

1. Tarehe ya Kuripoti Shule ya Polisi Moshi

Vijana wote wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 12 Juni 2025 hadi 14 Juni 2025. Muda wa kuripoti ni saa 2:00 asubuhi. Mtu yeyote atakayewasili baada ya tarehe 14 Juni 2025 hatapokelewa na atachukuliwa kuwa amejiondoa mwenyewe kwenye mafunzo.

2. Utaratibu wa Safari kwa Kanda na Mikoa

a) Vijana waliofanyiwa usaili Dar es Salaam (Vikosi vya Makao Makuu)

Watakutana tarehe 12 Juni 2025 saa 12:00 asubuhi katika Uwanja wa Gwaride, Kambi ya Polisi Kilwa Road, kwa ajili ya kuanza safari ya pamoja kwenda Moshi.

b) Vijana wa Mikoa ya Tanzania Bara

Wanatakiwa kuripoti kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa husika walikofanyia usaili tarehe 11 Juni 2025 saa 2:00 asubuhi, ili kupata maelekezo ya safari ya kwenda Moshi.

c) Vijana wa Zanzibar (Unguja na Pemba)

Wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe 11 Juni 2025 saa 2:00 asubuhi kwa maelekezo ya safari.

3. Vifaa Muhimu vya Kuambatana Navyo

Vijana wote wanapaswa kufika Moshi wakiwa na vifaa vifuatavyo:

Vifaa vya Mavazi na Malazi:

  • Traki suti ya bluu yenye ufito mweupe
  • Fulana nyeupe isiyo na maandishi
  • Raba, soksi nyeusi
  • Bukta mbili (2) za rangi ya bluu
  • Sanduku la chuma (tranka) la bluu
  • Chandarua cheupe cha duara
  • Shuka 4 za bluu mpauko (jozi mbili)
  • Pasi ya mkaa
  • Blanketi moja la kijivu (lisilo na maua wala duvet)

Vifaa vya Chakula:

  • Kikombe cha plastiki (cream light)
  • Sahani moja ya chuma (steel dish plate)

Vifaa vya Usafi:

  • Sururu moja yenye mpini
  • Ndoo mbili ndogo
  • Fagio la chelewa

Vinginevyo:

  • Kadi ya NHIF au Tsh. 50,400/= kwa wasio na bima
  • Vyeti halisi vya taaluma, cheti halisi cha kuzaliwa
  • Kadi ya NIDA au namba ya utambulisho wa taifa (NIDA)
  • Nakala za NIDA za wazazi au watu wa karibu (baba, mama, babu, nk.)
  • Picha ndogo za passport 6 (background ya bluu)
  • Nakala 5 kwa kila cheti kilichoainishwa
  • Fedha za kujikimu

4. Marufuku ya Simu za Mkononi

Simu za mkononi haziruhusiwi chuoni. Mwanafunzi yeyote atakayekutwa na simu atafukuzwa mafunzo mara moja. Shule itatoa utaratibu wa mawasiliano.

5. Orodha ya Majina

Orodha kamili ya vijana waliochaguliwa imeambatishwa na inapatikana kupitia kiungo rasmi cha Jeshi la Polisi:
 TANGAZO_LA_KURIPOTI_SHULE_YA_POLISI_MOSHI.pdf

Imetolewa na:
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania
Makao Makuu ya Polisi
S.L.P 961,
DODOMA
 01 Juni 2025

TANGAZO_LA_KURIPOTI_SHULE_YA_POLISI_MOSHI.pdf

https://polisi.go.tz:8000/media/matangazo/TANGAZO_LA_KURIPOTI_SHULE_YA_POLISI_MOSHI.pdf

Makala Nyingine:

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.