Timu zilizofuzu Makundi Kombe La Shirikisho Africa 2025/2026 CAF

Timu zilizofuzu Makundi Kombe La Shirikisho Africa 2025/2026 CAF,   Kwenye makala hii tutaona orodha ya Timu zilizofuzu hatua ya makundi CAFCL  Kombe La Shirikisho Africa.

Ni rasmi sasa! Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetangaza majina ya vilabu 16 vilivyofanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya CAF Confederation Cup 2025/26.

Mashindano haya yanatarajiwa kuwa moto wa kuotea mbali, yakihusisha vigogo wa zamani pamoja na sura mpya zenye kiu ya mafanikio makubwa.

Orodha ya Timu 16 Zilizofuzu Hatua ya Makundi

Na. Timu Nchi
1 Azam FC Tanzania
2 Singida Black Stars Tanzania
3 Zamalek SC Misri
4 CR Belouizdad Algeria
5 Wydad AC Morocco
6 Maniema Union DRC Congo
7 Zesco United Zambia
8 USM Alger Algeria
9 FC San Pedro Ivory Coast
10 OC Safi Morocco
11 Kaizer Chiefs Afrika Kusini
12 Stellenbosch FC Afrika Kusini
13 AS Otohô Congo Brazzaville
14 Djoliba AC Mali
15 Nairobi United Kenya
16 Al Masry SC Misri

🇹🇿 Fahari ya Tanzania

Tanzania imeandika historia kwa mara nyingine, baada ya Azam FC na Singida Black Stars kuingia hatua ya makundi kwa kishindo kikubwa.
Mashabiki wa soka nchini wamefurahia mafanikio haya, wakiamini kuwa mwaka huu huenda nchi hiyo ikatoa bingwa mpya wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Vigogo wa Afrika Waja Kivingine

Vilabu vikongwe kama Zamalek SC, Wydad AC, na USM Alger vinakuja na uzoefu mkubwa wa michuano ya kimataifa, vikiahidi kufanya mashindano haya kuwa ya kusisimua zaidi.

Kwa upande mwingine, timu kama Stellenbosch na Nairobi United zinawakilisha kizazi kipya cha vilabu vinavyopanda kwa kasi barani Afrika.

Matarajio

Hatua ya makundi inatarajiwa kuanza Novemba 2025, ambapo timu zitapangwa kwenye makundi manne (A–D), kila moja likiwa na timu nne.

Mashabiki wanatarajia mechi kali, hasa zile zitakazozikutanisha vigogo wa Afrika Mashariki dhidi ya mabingwa wa Kaskazini na Kusini mwa Afrika.

Makala Nyingine: