Tangazo La Nafasi Za Kazi Wakala Wa Usajili Wa Biashara Na Leseni (BRELA) 20-05-2025, Kwa niaba ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapokea maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa stahiki ili kujaza nafasi mbili (2) kama zilivyoainishwa hapa chini:
1. Mkurugenzi wa Leseni – Nafasi 1
Waajiri: BRELA
Anaripoti kwa: Mtendaji Mkuu wa BRELA
Wasimamizi Wanaohusika: Meneja – Kitengo cha Leseni za Biashara na Meneja – Kitengo cha Leseni za Viwanda
Majukumu:
- Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Leseni za Viwanda ya mwaka 1967 na Sheria ya Leseni za Biashara ya mwaka 1972.
- Kushauri juu ya masuala yanayohusu leseni za viwanda na biashara.
- Kusimamia shughuli zote za Idara ya Leseni.
- Kuratibu maandalizi ya mapendekezo kwa ajili ya Bodi ya Leseni za Viwanda.
- Kushauriana na taasisi nyingine juu ya masuala ya leseni.
- Kuandaa mipango mikakati, bajeti, na ripoti za utendaji kazi.
- Kupitisha na kufuta leseni inapobidi.
Sifa za Mwombaji:
- Shahada ya Uzamili katika fani ya Uchumi, Sheria, Biashara, Masoko, Takwimu, Biashara ya Kimataifa au fani zinazohusiana.
- Uzoefu wa kazi usiopungua miaka 10, ikiwa ni pamoja na miaka 2 katika nafasi ya uongozi.
- Umri usiozidi miaka 45 (isipokuwa kwa waajiriwa wa Umma).
2. Mkuu wa Kitengo cha Usajili wa Biashara – Nafasi 1 (Tangazo la Marudio)
Waajiri: BRELA
Anaripoti kwa: Mtendaji Mkuu wa BRELA
Majukumu:
- Kusimamia na kutoa ushauri juu ya usimamizi wa kumbukumbu.
- Kuhifadhi kumbukumbu za kielektroniki na za karatasi kwa kuzingatia sera na miongozo ya Serikali.
- Kusimamia uainishaji wa mafaili, sajili za majina ya biashara, kampuni, leseni na alama za biashara.
- Kusimamia mzunguko wa mafaili, kutunza kumbukumbu za barua na nyaraka zote muhimu.
- Kuratibu uhifadhi na uondoaji wa kumbukumbu.
- Kusimamia upangaji wa mafaili na usimamizi wa mifumo ya uhifadhi wa kumbukumbu.
Sifa za Mwombaji:
- Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Kumbukumbu, Nyaraka au fani zinazofanana.
- Uzoefu wa kazi usiopungua miaka 8, akiwa angalau katika ngazi ya juu (Senior level).
- Umri usiozidi miaka 45 (isipokuwa kwa waajiriwa wa Umma).
Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
- Waombaji wote wawe raia wa Tanzania.
- Waambatishe wasifu (CV) wa kisasa wenye mawasiliano sahihi.
- Wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kutaja hali yao katika mfumo wa maombi.
- Waambatishe nakala zilizothibitishwa za vyeti vya elimu, kitaaluma, usajili, na cheti cha kuzaliwa.
- Vyeti vya elimu ya sekondari kutoka nje ya nchi vihakikiwe na NECTA; vya elimu ya juu vihakikiwe na TCU/NACTE.
- Maombi yaandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza, yatiwe saini na yaelekezwe kwa:
Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira, S.L.P. 2320, Jengo la Utumishi, Chuo Kikuu cha Dodoma – Dodoma.
Mwisho wa kutuma maombi:
Tarehe 02 Juni, 2025.
Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa ajira wa serikali:
http://portal.ajira.go.tz/
Imetolewa na:
KATIBU – SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Makala Nyingine: