Ajira

Tangazo La Nafasi Za Kazi – Halmashauri Ya Wilaya Ya Mlele (Mei 2025)

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa kujaza nafasi mbalimbali za ajira kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kufuatia kibali kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kumb. Na. KTV/MLDC/S.10/2 | Tarehe: 25/05/2025

1.0 NAFASI ZINAZOTANGAZWA

1.1 Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II (Nafasi 3)

Majukumu ni pamoja na kuchapa nyaraka, kupokea wageni na kushughulikia matatizo yao, kutunza kumbukumbu za vikao, safari, na kazi za mkuu wa idara. Pia atatakiwa kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao pamoja na kuandaa mahitaji ya vifaa vya ofisi.

Sifa za mwombaji ni kuhitimu kidato cha nne au sita, kuwa na Stashahada ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili, kuwa na uwezo wa kuchapa maneno 100 kwa dakika kwa Kiswahili na Kiingereza, pamoja na ujuzi wa programu za kompyuta kama Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email na Publisher.
Ngazi ya mshahara ni TGS C.

1.2 Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja II (Nafasi 3)

Majukumu ni pamoja na kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka, kusambaza majalada kwa watendaji, kutafuta kumbukumbu, na kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya taasisi.

Sifa ni kuhitimu kidato cha nne au sita, kuwa na Diploma (NTA Level 6) katika fani ya Masjala kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na awe na ujuzi wa kompyuta.
Ngazi ya mshahara ni TGS C.

1.3 Dereva Daraja II (Nafasi 3)

Majukumu ni pamoja na kukagua usalama wa gari kabla na baada ya safari, kuendesha magari ya serikali kwa safari za kikazi, kufanya matengenezo madogomadogo, kusambaza nyaraka, kujaza taarifa za safari, na kufanya usafi wa gari.

Sifa ni kuwa na cheti cha kidato cha nne, kuwa na leseni ya daraja E au C, kuwa na uzoefu wa kuendesha kwa mwaka mmoja bila kusababisha ajali, na kuwa amehitimu mafunzo ya msingi ya udereva kutoka VETA au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Ngazi ya mshahara ni TGS B.

2.0 MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  1. Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45, isipokuwa kwa walioko kazini Serikalini.
  2. Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kutuma maombi na waeleze aina ya ulemavu waliokuwa nao kwenye mfumo.
  3. Waombaji waambatishe wasifu binafsi (CV), anuani sahihi, namba ya simu, barua pepe, na majina ya wadhamini watatu.
  4. Waombaji waliopo kwenye utumishi wa umma katika nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.
  5. Maombi yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na mwanasheria au wakili, ikiwemo cheti cha kidato cha nne/sita, vyeti vya taaluma, vyeti vya kompyuta na vyeti vya kitaaluma.
  6. Hati za matokeo, provisional results, statement of results au result slips hazitakubaliwa.
  7. Waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vimehakikiwa na kuthibitishwa na TCU, NECTA au NACTE.
  8. Wastaafu hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali kutoka Katibu Mkuu Kiongozi.
  9. Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
  10. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 03 Juni, 2025.

3.0 NAMNA YA KUTUMA MAOMBI

Barua ya maombi ya kazi iwe imeandikwa na kusainiwa, iambatane na vyeti vyote muhimu na ipelekwe kwa anuani ifuatayo:

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele,
S.L.P 686.

Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kwa kutumia anuani:
👉 https://portal.ajira.go.tz

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu hayatafanyiwa kazi.

Imetolewa na:
Sigilinda M. Mdemu
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele

250526171500 TANGAZO LA AJIRA MPYA 202425 MLELE DC .pdf

Makala Nyingine:

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.