TaESA Login Portal (Mfumo wa Ajira) Jinsi ya Kujisajili TAESA, TaESA Jobs Gateway (Tanzania Employment Services Agency)
Mwongozo huu unalenga kutoa maelekezo kwa watumiaji waliosajiliwa kwenye Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Ajira (EMIS), unaotumiwa na TaESA kusaidia watafuta ajira.
1. Kuhusu Mfumo
EMIS ni mfumo wa wavuti ulioundwa kusaidia utoaji wa huduma kwa watafuta ajira. Unapatikana kwa kutumia kompyuta au simu yenye kivinjari na muunganisho wa intaneti.
Walengwa
Mwongozo huu ni kwa ajili ya watafuta ajira ili kuwawezesha kutumia mfumo kwa ufanisi.
Vipengele Muhimu vya Mfumo
- Usajili wa akaunti
- Ufikaji wa mfumo
- Usajili wa mtafuta ajira
- Usimamizi wa ajira za kuvuka mipaka
2. USAJILI WA AKAUNTI
- Fungua kivinjari na andika: jobs.kazi.go.tz
- Bonyeza Login kisha Create Account
- Jaza taarifa zote zinazohitajika
- Bonyeza Create Account
- Nenda kwenye barua pepe yako kuthibitisha akaunti
USAJILI WA MTAFUTA AJIRA
Chagua Aina ya Akaunti
- Ingia kwenye mfumo
- Chagua Jobseeker
- Bonyeza Proceed
Hakiki Namba ya NIDA na Jaza Taarifa
- Weka namba ya NIDA
- Bonyeza Verify NIDA
- Jaza taarifa zote zinazohitajika
- Bonyeza Register
Hatuwa Muhimu za Kujaza
- Mapendeleo ya Mafunzo
- Watu wa Marejeo (Referees) watatu
- Ujuzi mbalimbali
- Uwezo wa Lugha
- Sifa za Elimu
- Viambatanisho vya Elimu
- Mapendeleo ya Kazi (angalau 2 hadi 4)
- Picha ndogo ya pasipoti
- Taarifa za Uzoefu wa Kazi (si lazima)
- Sifa za Kitaaluma (si lazima)
- Taarifa za JKT au Mafunzo mengine (si lazima)
- Wasilisha Wasifu (CV)
4. UFIKAJI NA UTUMIAJI WA MFUMO
- Ingia kwa kutumia anwani ya barua pepe na nywila uliyosajili nayo
- Tumia menyu za mfumo kusafiri na kupata huduma
Kuondoka Kwenye Mfumo
- Bonyeza mshale chini kando ya jina lako
- Chagua Logout
Badilisha Nenosiri
-
Chagua Change Password, ingiza nenosiri la zamani, jipya, na thibitisha
Umesahau Nenosiri?
- Bonyeza Reset Password, ingiza barua pepe yako
- Fuata maelekezo uliyotumiwa kupitia barua pepe
5. USAJILI WA NAFASI ZA AJIRA ZA NJE YA NCHI
- Ingia kwenye mfumo, chagua Cross Border
- Bonyeza Add Opportunity
- Jaza taarifa, ambatanisha nyaraka, ongeza maelezo ya kazi
- Lipa kwa kutumia namba ya malipo iliyotolewa
- TaESA itakagua na kukubali/kukataa ombi
6. MAFUNZO
- Mtafuta ajira aliyethibitishwa anaweza kuweka nafasi ya kuhudhuria mafunzo
- Pia anaweza kuomba ratiba maalum ya mafunzo
7. USAILI
-
Mtafuta ajira anaweza kuona alama za usaili baada ya kufanya mahojiano
8. MAOMBI YA AJIRA
- Fungua fursa kwenye mfumo, bonyeza Apply
- Thibitisha kutuma maombi yako
- Angalia hali ya maombi yako, fanya mtihani wa tathmini (Aptitude Test)
- Angalia cheti cha mafunzo au nafasi ya kazi (Placement Certificate)
Ili kuanza mchakato wa kujisajili na TAESA, tembelea tovuti rasmi kupitia jobs.kazi.go.tz/portal.
Makala Nyingine:
- Nafasi za Kazi Ajira Portal, Serikalini na UTUMISHI 2025
- Mfumo Wa Ajira TRA (recruitment.tra.go.tz) recruitment Portal 2025
- ESS Utumishi (Watumishi Portal)
- Jinsi Ya kujisajili NIDA online (Kitambulisho Cha Taifa)
- Jinsi Ya Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu 2025 Matandaoni