{"id":14508,"date":"2026-05-02T19:22:52","date_gmt":"2026-05-02T16:22:52","guid":{"rendered":"https:\/\/kaziforums.com\/?p=14508"},"modified":"2026-05-02T19:22:52","modified_gmt":"2026-05-02T16:22:52","slug":"nafasi-za-kazi-halmashauri-ya-manispaa-ya-tabora-23-08-2024","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/elimuforum.com\/sw\/nafasi-za-kazi-halmashauri-ya-manispaa-ya-tabora-23-08-2024\/","title":{"rendered":"Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Manispaa Ya Tabora 23-08-2024"},"content":{"rendered":"<p>Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Manispaa Ya Tabora 23-08-2024, Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023\/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97\/288\/01\/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.<\/p>\n<p>Kufuatia kibali hicho, Mkurugenzi anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:<\/p>\n<h3>1.0 DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 05)<\/h3>\n<p><strong>1.1 Kazi na Majukumu<\/strong><\/p>\n<ul>\n<li>Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.<\/li>\n<li>Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi.<\/li>\n<li>Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.<\/li>\n<li>Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.<\/li>\n<li>Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari (log book).<\/li>\n<li>Kufanya usafi wa gari.<\/li>\n<\/ul>\n<p><strong>1.1.1 Sifa za Kuajiriwa<\/strong><\/p>\n<ul>\n<li>Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI).<\/li>\n<li>Awe na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari, ambayo ameifanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.<\/li>\n<li>Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.<\/li>\n<\/ul>\n<p><strong>1.1.2 Ngazi ya Mshahara<\/strong><\/p>\n<ul>\n<li>Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali, yaani TGS B.<\/li>\n<\/ul>\n<h3>1.2 MTENDAJI WA MTAA III (NAFASI 05)<\/h3>\n<p><strong>1.2.1 Majukumu ya Kazi<\/strong><\/p>\n<ul>\n<li>Kuwa Afisa Masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mtaa.<\/li>\n<li>Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao.<\/li>\n<li>Kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Mtaa.<\/li>\n<li>Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji mipango ya maendeleo ya Mtaa.<\/li>\n<li>Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Mtaa.<\/li>\n<li>Kutafsiri na kusimamia sera, sheria, na taratibu.<\/li>\n<li>Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo la kazi na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.<\/li>\n<li>Kuongoza wakuu wa vitengo vya kitaaluma katika jamii.<\/li>\n<li>Kusimamia, kukusanya, na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Mtaa.<\/li>\n<li>Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu katika Mtaa.<\/li>\n<li>Kusimamia utungaji wa sheria ndogondogo za Mtaa.<\/li>\n<li>Kupokea, kusikiliza, na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.<\/li>\n<li>Kusimamia ukusanyaji wa mapato ndani ya Mtaa na kusoma mapato na matumizi kila baada ya miezi miwili.<\/li>\n<\/ul>\n<p><strong>1.2.2 Sifa za Kuajiriwa<\/strong><\/p>\n<ul>\n<li>Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI).<\/li>\n<li>Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada\/Cheti (NTA LEVEL 5) katika mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.<\/li>\n<\/ul>\n<p><strong>1.2.3 Ngazi ya Mshahara<\/strong><\/p>\n<ul>\n<li>Kwa kuzingatia ngazi za mshahara ya Serikali \u2013 TGS B.<\/li>\n<\/ul>\n<h3>1.3 MTENDAJI WA KIJIJI III (NAFASI 05)<\/h3>\n<p><strong>1.3.1 Majukumu ya Kazi<\/strong><\/p>\n<ul>\n<li>Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.<\/li>\n<li>Katibu wa Kamati ya Kijiji.<\/li>\n<li>Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Kijiji.<\/li>\n<li>Mshauri wa Kamati ya Kijiji kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Kijiji.<\/li>\n<li>Msimamizi wa utekelezaji wa Sheria ndogo na Sheria nyingine zinazotumika katika Kijiji.<\/li>\n<li>Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na umasikini katika Kijiji.<\/li>\n<li>Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi.<\/li>\n<\/ul>\n<p><strong>1.3.2 Sifa za Kuajiriwa<\/strong><\/p>\n<ul>\n<li>Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).<\/li>\n<li>Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada katika moja ya fani zifuatazo: Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii, na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.<\/li>\n<\/ul>\n<p><strong>1.3.3 Ngazi ya Mshahara<\/strong><\/p>\n<ul>\n<li>Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali \u2013 TGS B.<\/li>\n<\/ul>\n<h3>MASHARTI YA JUMLA<\/h3>\n<ol>\n<li>Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 hadi 45 isipokuwa kwa wale walioko kazini Serikalini.<\/li>\n<li>Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na kuainisha aina ya ulemavu walionao kwenye mfumo wa kuombea ajira.<\/li>\n<li>Waombaji waambatanishe maelezo binafsi (CV) yenye anuani, namba za simu zinazopatikana, na anuani ya barua pepe pamoja na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika.<\/li>\n<li>&#8220;Provisional,&#8221; &#8220;Testimonials,&#8221; &#8220;Statement of results,&#8221; na hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita hazitakubaliwa.<\/li>\n<li>Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria\/Wakili.<\/li>\n<li>Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.<\/li>\n<li>Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika kada tofauti, wapitishe barua zao za maombi kupitia waajiri wao.<\/li>\n<li>Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.<\/li>\n<li>Waombaji waambatanishe vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria\/Wakili (Cheti cha Kidato cha Nne, Kidato cha Sita, vyeti vya mafunzo mbalimbali).<\/li>\n<li>Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA, NACTVET).<\/li>\n<li>Uwasilishaji wa taarifa za kughushi utachukuliwa hatua za kisheria.<\/li>\n<li>Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.<\/li>\n<li>Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 03 Septemba 2024.<\/li>\n<\/ol>\n<h3><strong>MUHIMU:<\/strong><\/h3>\n<p>Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua iandikwe kwa:<\/p>\n<p><strong>Mkurugenzi wa Manispaa,<\/strong><br \/>\nHalmashauri ya Manispaa ya Tabora,<br \/>\nMtaa wa Ikulu,<br \/>\nBarabara ya Kiwanja cha Ndege,<br \/>\nS.L.P 174,<br \/>\n45182 TABORA.<\/p>\n<p>Maombi yote ya kazi yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: <a href=\"https:\/\/portal.ajira.go.tz\" target=\"_new\" rel=\"noopener\">https:\/\/portal.ajira.go.tz<\/a>.<\/p>\n<p>Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu hayatafanyiwa kazi.<\/p>\n<p><strong>Imetolewa na:<\/strong><\/p>\n<p><strong>MKURUGENZI WA MANISPAA,<\/strong><br \/>\n<strong>HALMASHAURI YA MANISPAA TABORA.<\/strong><\/p>\n<p><strong>Soma Zaidi:\u00a0<a href=\"https:\/\/elimuforum.com\/sw\/nafasi-za-kazi-halmashauri-ya-wilaya-ya-chamwino-25-08-2024\/\">Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Chamwino 25-08-2024<\/a><\/strong><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Manispaa Ya Tabora 23-08-2024, Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023\/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97\/288\/01\/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho, Mkurugenzi anakaribisha maombi kutoka kwa [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1288],"tags":[1324],"class_list":{"0":"post-14508","1":"post","2":"type-post","3":"status-publish","4":"format-standard","6":"category-ajira","7":"tag-halmashauri-ya-manispaa-ya-tabora"},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/elimuforum.com\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/14508","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/elimuforum.com\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/elimuforum.com\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/elimuforum.com\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/elimuforum.com\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=14508"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/elimuforum.com\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/14508\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":19771,"href":"https:\/\/elimuforum.com\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/14508\/revisions\/19771"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/elimuforum.com\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=14508"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/elimuforum.com\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=14508"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/elimuforum.com\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=14508"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}